Visit Sponsor

Written by 3:05 pm KITAIFA Views: 57

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAIBUKA MSHINDI WA PILI KUTOA TAARIFA KWA UMMA

Na Carren Mgonja

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeibuka mshindi wa pili kati ya Wizara kumi Bora kwa kutoa taarifa kwa Umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika kipindi cha mwaka 2023/2024.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ametangaza ushindi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mbele ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari na Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kilichofunguliwa leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo la pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari nchini limefunguliwa na Rais Samia na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari, mabalozi na miongoni mwa makatibu wakuu waliohudhuria ni wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally S. Gugu na Viongozi wengine wa Serikali.

About The Author

(Visited 57 times, 1 visits today)

Last modified: June 18, 2024

Close