Visit Sponsor

Written by 1:09 pm KITAIFA Views: 42

WIZARA YA MALIASILI YAJA KIDIGITALI

Mkurugenzi wa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Thereza Mugobi
(mwenye koti la kijani) akitembelea mabanda yenye wanyamapori kwenye
Maonesho ya SABA SABA jijini Dar es Salaam.

Wizara ya Malisili na Utalii imeamua kwenda na kasi ya mabadiliko ya
sayansi na Teknolojia kwa kuanza kutangaza Utalii kidigitali katika Maonesho
ya 47 Kibiashara ya Kimataifa Dar es Salaam, maarufu kama Saba Saba.
Akizungumza baada ya kutembelea banda la Wizara hiyo, Mkurugenzi wa
Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Thereza Mugobi amesema, hauwezi
kuongelea Utalii bila kuongelea mambo ya kidigitali na ndo maana Wizara
imeamua kwenda na mabadiliko hayo ya teknolojia yaliyopo duniani Kwa
Taasisi na Idara za Wizara hiyo Kutumia njia ya Kidijitali kuonesha Shughuli
na huduma zao mbalimbali.
“Kwenye mabanda yetu watanzania wataweza kuona Utalii wetu kwa kupitia
simu janja zao za mikononi (smartphone). Tuna QR Code kwenye kila banda
ambazo watanzania wataskani kwa ajili ya kupata vivutio vilivyopo Tanzania
nzima na kujua vivutio hivyo pamoja na huduma zinazotolewa na Taasisi
zetu” Amesema Dkt. Mugobi.
Katika Maonesho hayo, Wizara imejipanga vyema kuwahudumia wote
wanaofika katika banda hilo kwa kasi zaidi kupitia njia hiyo ya kisasa tofauti
na ilivyokuwa huko nyuma Taarifa nyingi zilikuwa zikitolewa kwenye
vipeperushi ambavyo ni mzigo kwa wageni.
Aidha Dkt. Mugobi ametoa wito Kwa wananchi kujitokeza Kwa wingi kujipatia
huduma mbalimbali kwenye Banda la Maliasili na Utalii ambazo ni njia sahihi
na rahisi ya kujipatia fursa mbalimbali kwenye sekta zilizopo chini ya Wizara
hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Ndugu Damasi Mfugale
amefurahishwa na ufanisi wa kutangaza Utalii kidigitali katika maonesho
hayo ya SABASABA na kusema watahakikisha kila Taasisi ya Wizara
itatangaza Utalii kisasa Zaidi.
Bw. Luca Hakili, Mkazi wa Jiji la Jijini Dar es Salaam licha ya kupendezwa na
huduma Zinazotolewa na Taasisi mbalimbali za Wizara ya Maliasili na Utalii,
amezipongeza kwa ufanisi wa taasisi hizo katika kutangaza maliasili zilizopo
Tanzania Kisasa zaidi.
Bw. Hakili ameongeza kuwa kwake imekuwa ni fursa muhimu ya kujua
rasilimali lukuki zilizopo nchini na fursa zilizopo kwenye Utalii, Misitu,
Wanyamapori pamoja, Malikale na Taasisi zingine.

Pamoja na Mambo mengine, katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
wakazi wa Dar es Salaam wamepata fursa ya kuangalia Filamu ya “Tanzania
The Royal Tour” iliyosimamiwa na Mhe. Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.

Akizungumza baada ya kuangalia filamu hiyo Mtoto, Feisal Seif
amefurahishwa kupata fursa ya kuangalia filamu hiyo na kuwataka watoto
wenzake kuja kuangalia na kujifunza mambo mengi kuhusu Utalii, uhifadhi,
maliasili na kuja kuona wanyapori.

Mkurugenzi wa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Thereza Mugobi
(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Masoko ya Ndani Bodi ya
Utalii Tanzania, Bw. Felix John baada ya kutembelea Banda la Wizara hiyo
kwenye Maonesho ya SABA SABA jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii, Bw. Damasi Mfugale (mwenye miwani)
akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa Banda la Wizara ya Maliasili na
Utalii,Bw. Felix John baada ya kutembelea Banda la Wizara hiyo kwenye
Maonesho ya SABA SABA jijini Dar es Salaam.

About The Author

(Visited 42 times, 1 visits today)

Last modified: July 1, 2023

Close