Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ziara iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea Kusini imetengeneza mahusiano mazuri na kuchangia kupatikana kwa fedha kwa ajili ya mradi mikubwa wa maji safi na usafi wa mazingira.
Akizungumza leo Disemba 16,2024 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Mfumo wa Kutibu Majitaka Katika Jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Ziara ya Waziri Aweso na timu nzima ya sekta ya Maji Nchini Korea Kusini.
Aidha Waziri Aweso amesema “baada ya kupata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya Korea Kusini kwa muda mfupi sana baada ya kumaliza na mimi nimepata nafasi hivi karibuni kwenda haijafika hata wiki tumepata zaidi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 240 kwa ajili ya uwekezaji kwenye maji taka”
Ameongeza kuwa hiyo inathibitisha mahusiano mazuri na urafiki wa thamani uliopo baina ya nchi hizi mbili ikichangiwa na ziara ya Rais Samia nchini humo pamoja na yeye mwenyewe ” sio jambo jepesi kwenda na muda mfupi huo huo ukapata pesa hii ni kazi kubwa hii, ni kazi nzuri ya mahusiano na kujitoa kwake Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan”
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemshukuru Balozi wa Korea Kusini nchini Eunju Ahn kwa kuwa sehemu kubwa ya kusaidia kupatikana kwa miradi hiyo “nipende kumshukuru sana Balozi wa Korea Mheshimwa Ahn haya mafanikio tuliyioyapata nii kutokana na ushirikiano mkubwa huwezi ukafanya kazi peke yako”
Mradi huo utagharimu zaidi ya dola milioni 90 sawa na bilioni 170 mpaka utakapokamilika ambapo Waziri Aweso amesema itakuwa suluhisho kubwa kwa changamoto za maji katika hilo “kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam kutoka asilimia 45 ya sasa hadi asilimia 65”
About The Author
Last modified: December 16, 2024