Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepanga
kuchambua Miswada miwili ya Sheria iliyopelekwa kwenye Kamati hiyo.
Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
(Na.4) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellanaous Amendments)
(No.4)Bill, 2023] na Muswada ya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
za Sekta ya Sheria wa Mwaka 2023 [The Legal Sector Laws (Miscellaneous
Amendments) Bill, 2023].
Katika kutekeleza jukumu hilo na kwa mujibu wa Kanuni ya 97 (2) ya Kanuni
za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023, Kamati itasikiliza na kupokea
maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya Alhamisi tarehe 19 Oktoba, 2023
saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Frank Mfundo, Ghorofa ya 5 Jengo la
Utawala, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.
Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepanga kufanya
Mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu Azimio la Bunge la
Mapendekezo ya Tanzania Kuridhia Kujiunga na Mkataba wa Wakala wa
Kimataifa wa Nishati Jadidifu wa Mwaka 2009 (Statute of The International
Renewable Energy Agency – Irena). Kamati inatekeleza jukumu hilo kwa
mujibu wa Kanuni ya 97 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la
Februari, 2023
Kamati itasikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya
Alhamisi tarehe 19 Oktoba, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa
Msekwa kwenye Jengo la Pius Msekwa, Jijini Dodoma.
Kamati zinawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Miswada na Azimio hilo
kufika na kuwasilisha maoni yao kabla kupelekwa katika hatua nyingine.
Vilevile Kamati zitapokea maoni kwa njia ya Posta au Barua Pepe kwa anuani
ifuatayo: –
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 941,
41105 Tambukareli,
DODOMA.
Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz
Miswada na Azimio hilo vinaweza kupakuliwa katika Tovuti ya Bunge,
www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua
pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa
ajili ya hatua za kiutawala.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
7 Oktoba, 2023.
About The Author
Last modified: October 7, 2023