Kuhusu tetesi za uwepo wa #COVID19; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanya kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la??
Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki ya tarehe 6 – 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona. Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19
Wizaraย ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili.
Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za Afya na Usafi
About The Author
Last modified: May 30, 2023