Visit Sponsor

Written by 4:20 pm KITAIFA Views: 17

WAZIRI SILAA AFUNGUA MILANGO KWA WADAU WA HABARI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa leo Novemba 21, 2024 amekutana na wadau balimbali wa Sekta hiyo ili kujadiliana na kufahamiana zaidi kuelekea vikao kazi pangwa hapo baadae vya kuijengea na kuimarisha sekta hiyo.

Kupitia mkutano huo uliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Jijini Dar es salaam, Waziri Silaa amesema kuwa  yeye kama Waziri wa Habari anafanya kazi kwa sera ya mlango wazi na kwamba wakati wowote wadau wa sekta hiyo wanakaribishwa.

“Mimi binafsi Waziri wa Habai, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ninaomba kuwataarifu na kuendelea kuwaeleza kwamba ninafanya kazi na ‘open door polic’, kwahiyo wakati wowote CoRI, wanachama wa CoRI  mmoja mmoja, lakini vyombo vya habari vyote 1,023 wakati wote vione milango iko wazi kuweza kuifikia wizara au kumfikia waziri kama waziri katika kubadilishana mawazo na kujengeana uelewa na kutengeneza mazingira ambayo Taasisi za Habari na Wizara ya Habari inaweza kuendelea kufanya kazi kwa pamoja”, amesema Silaa.

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya Waziri Silaa kufungua kikao hicho, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), ambaye pia  ni Mwenyekiti wa CoRI (Coalition on the Right to Information au Umoja wa haki ya kupata taarifa), Ernest Sungula amesema wako hapo kukutana na waziri ili kushirikishana changamoto, mafanikio na baada ya mazungumzo hayo kutakua na vikao vingine vya kikazi zaidi.

 Sungura ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mabaraza huru ya Habari Afrika amesema kuwa tangu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ateuliwe kubeba dhamana ya kuongoza wizara hiyo, wao kama wadau wa habari wanaoongoza wanachama waliona ni muhimu wakutana naye ili awafahamu vizuri majukumu yao na jinsi wanavyofanya kazi, wakamuandikia barua, akawajibu yuko tayari.

“Leo tuko hapa kukutana na Mhe. Waziri kwanza kutufahamu, kazi zetu, kushirikishana changamoto na mafanikio, na kazi ambazo tumekuwa tukizifanya kukuza Sekta yetu ya Habari hapa nchini, baada ya mazungumzo tunatarajia tutakuwa na vikao vingine vya kikazi zaidi,” Sungula.

About The Author

(Visited 17 times, 1 visits today)

Last modified: November 21, 2024

Close