Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpogeza Rais wa Madagascar Andry Rajoelina katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa Ikulu ya Antananarivo. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za kumwapisha Rais huyo zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamsina, Desemba 16, 2023. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, wa pili kulia ni Mke wa Rais wa Madagascar, Mialy Rajoelina na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, Wakili Stephen Byabato. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina akihutubia Taifa baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tatu katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi katika sherehe za kumwapisha Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina akiwapungia wananchi alipowasili kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tatu, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina akiwa na mkewe, Mialy Rajoelina, na watoto wao Arena Rajoelina na Ilonstoa Rajoelina (kulia) baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tatu katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
About The Author
Last modified: December 16, 2023