Visit Sponsor

Written by 6:01 pm KITAIFA Views: 11

WAZIRI MKUU AKABIDHI TUZO KWA JKCI KWA KUIBUKA MSHINDI WA KWANZA WA JUMLA MAONESHO YA SABASABA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa jumla katika
maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela
Muhozya wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika
Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo yenye
washiriki 3514 kutoka ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda baada ya Taasisi hiyo kuibuka
mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam (SABASABA) wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.

About The Author

(Visited 11 times, 1 visits today)

Last modified: July 5, 2023

Close