Visit Sponsor

Written by 5:09 pm KITAIFA Views: 14

WAZIRI MASAUNI: POLISI LITAMDHIBITI MUHARIFU YEYOTE BILA KUJALI NAFASI YAKE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kushoto ni IGP Camilius Wambura

Jeshi la polisi nchini litamchukulia hatua mtu yeyote atakayefanya uharifu bila kujali nafasi yake, iwe anafanyakazi Serikalini, kwa mtu binafsi, kwenye chombo cha usalama au kwingineko, lengo ni kutekeleza majuku yake ya msingi ya kulinda raia na mali zao.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 4, 2024 baada ya kumalizika kwa kikao kazi kati ya wizara yake na makamanda wa jeshi la Polisi nchini.

“Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha inaliwezesha jeshi la Polisi nchini kuweza kufanya kazi zake vizuri na jeshi la Polisi linafanya jitihada kubwa kuhakikisha linatekeleza majuku yake ya msingi ya kulinda raia na mali zake, lakini niwahakikishie kwamba tukio lolote la kiharifu ambalo limefanywa na mtu yeyote ikiwemo hayo matukio ambayo yamejitokeza hakuna hata tukio moja ambalo hakuna hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa, iwe tukio limefanywa na raia au na mtu mwingine yeyote. Hilo ni jambo ambalo nataka niwahakikishie wanachi wawe na imani na Serikali yao, wawe na imani na jeshi lao”, alisema Masauni.

Aidha Waziri Masauni ambaye awali alilipongeza jesho hilo kwa kazi kubwa wanayofanya na nchi kuendelea kuwa salama amesema kuwa hata matukio yote ya kiharifu ambayo yametokea au yalitokea na kuvuta hisia katika jamii hakuna ambalo halijachukuliwa hatua madhubuti na zinaendelea kuchukuliwa. “Chamsingi kikao chetu kimeenda vizuri na mwisho tumepeana maelekezo ya kuelekea mwaka 2024/25”, amesema.   

About The Author

(Visited 14 times, 1 visits today)

Last modified: January 4, 2024

Close