Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akizungumza jambo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Bi. Maria Helena Semedo mara baada ya
kufanyika Mkutano wa Uwili wakati wa Mkutano wa Sita wa Baraza wa
Mazingira Duniani (UNEA6) jijini Nairobi nchini Kenya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo ameliomba Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO)
kuendelea Kuunga mkono mipango ya Serikali ya Tanzania katika usimamizi
wa mazingira na kupambana na athari za mabadilko ya Tabianchi.
Pia, ameolimba shirika hilo kuisaidia Tanzania kitekenolojia, ubunifu, mafunzo
na masuala ya kifedha kwa miradi ya maendeleo, katika Sekta ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi hususan Ajenda 10/30.
Ametoa ombi hilo alipokutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO Bi. Maria
Helena Semedo katika Mkutano wa Uwili jijini Nairobi nchini Kenya wakati wa
Mkutano wa Sita wa Baraza wa Mazingira Duniani (UNEA6).
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2024/03/1-1024x617.jpg)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula
na Kilimo Duniani (FAO) Bi. Maria Helena Semedo (hayupo pichani) katika
Mkutano wa Uwili wakati wa Mkutano wa Sita wa Baraza wa Mazingira Duniani
(UNEA6) jijini Nairobi nchini Kenya. Kulia ni Afisa Mazingira Mwandamizi Ofisi
ya Makamu wa Rais, Simeon Shimbe.
Katika kikao hicho kilicholenga kuimarisha uhusiano baina ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na FAO, Dkt. Jafo amelishukuru kwa kazi kubwa
wanayofanya nchini tangu Tanzania ijiunge na shirikia hilo mwaka 1962 na
tangu shirika hilo lilipofungua Ofisi zake nchini mwaka 1977.
Ameongeza kuwa FAO imekuwa ikishirikiana vyema na Tanzania katika
kujengea uwezo wataalamu wa Serikali, kusaidia katika usalama wa chakula
sambamba na sekta ya Kilimo, Mazingira na masuala mbalimbali ya
kimaendeleo.
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2024/03/3-1024x484.jpg)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Bi. Maria
Helena Semedo (katikati) mara baada ya Mkutano wa Uwili wakati wa
Mkutano wa Sita wa Baraza wa Mazingira Duniani (UNEA6) jijini Nairobi nchini
Kenya.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu Bi. Semedo amemuhakikisha
Waziri Dkt. Jafo na Serikali ya Tanzania kwamba FAO itaendelea kudumisha
ushirikiano wao kwa kuweka nguvu katika sekta ya Mazingira.
Halikadhalika ameihakikishia Tanzania kuwa shirika litaendeleza utekelezaji wa
mipango mbalimbali ya maendeleo hususan kuongeza tija katika kilimo ili
Tanzania iweze kufikia malengo iliyojiwekea.
Itakumbukwa kuwa Mkutano UNEA6 huo uliofanyika Februari 26 hadi MNachi
mosi, 2024 ulichagizwa na kaulimbiu ‘Juhudi Madhubuti, Jumuishi na Endelevu
za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, Uharibifu wa Bioanuai na Uchafuzi‘.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri Dkt. Jafo akiambatana na Naibu
Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan
Mitawi pamoja na wataalamu kutoka Ofisi hiyo.
About The Author
Last modified: March 4, 2024