Visit Sponsor

Written by 2:15 pm KITAIFA Views: 5

Watuhumiwa wa Ubakaji na ulawiti wafungwa Maisha Jela,280 vifungo mbalimbali

Na Mwandishi JESHI LA POLISI ARUSHA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari, 2025 hadi Februari 2025 lilifanya operesheni dhidi ya uhalifu na wahalifu na kufanikiwa kukamata watuhumiwa mbalimbali na kuwafikishwa Mahakamani.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamjzi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa kwa upande wa makosa ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 15 na kuwafikisha mahakamani, ambapo kati yao 10 walikamatwa kwa tuhuma za ubakaji na wengine 05 kwa tuhuma za ulawiti

Ameongeza kuwa baada ya kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za ubakaji, Watuhumiwa 03 walihukumiwa vifungo vya maisha Jela, 01 kifungo cha miaka 30. Aidha mtuhumiwa 01 amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mwingine 01 kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za ulawiti. Watuhumiwa wengine kesi zao zipo katika hatua mbalimbali. 

SACP Masejo amebainisha kuwa Kupitia misako dhidi ya dawa za kulevya walifanikiwa kukamata Watuhumiwa 26 wakiwa na Mirungi Kilogramu 196.4, Watuhumiwa 22 wakiwa na Bhangi kilogramu 32 pamoja na kuteketeza zaidi ya hekari 10 za bhangi.

Aidha amefafanua kuwa watuhumiwa wote wa Dawa za kulevya tayari wamefikishwa Mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.

Vilevile kamanda Masejo ameeleza kuwa Kwa upande wa mapambano dhidi ya ujangili, walifanikiwa kukamata watuhumiwa 02 wakiwa na nyama ya Nungunungu kilogramu 20 ambapo tayari wamefikishwa Mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.

Sambamba na hayo amesema kuwa kwa kipindi hicho walifanikiwa kukamata Watuhumiwa 38 wakiwa na pombe ya Moshi lita 172 na mitambo 04 ya kutengenezea pombe hiyo ambapo watuhumiwa wote tayari wameshafikishwa Mahakamani kwa taratibu za kisheria huku watumiwa 202 wa makosa ya wizi wakikamatwa katika operesheni hiyo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha likatoa rahi kwa kwa baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kuacha mara moja vitendo hivyo kwani tutawakamata na kuchukua hatua za kisheria dhidi yao Pamoja na madereva wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: February 18, 2025

Close