Visit Sponsor

Written by 2:37 pm KITAIFA Views: 8

WATUHUMIWA 7 MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA DCEA YATOA RAI KWA WENYE NYUMBA WANAPOPANGISHA VYUMBA ZAO

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya DCEA Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Dola,imekamata jumla ya kilogram 2,207,56 za dawa za kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya Katika mikoa ya Tanga na Dar es salaam

Akizungumza na Mwandishi wa habari jijini dar es salaam Tarehe 25 Novemba 2024 Kamishna Mkuu wa DCEA Kamshna Aretas Lyimo Amesema watuhumiwa saba wanashikiliwa Kwa kuhusishwa na dawa hizo na kati ya dawa hizo zilizokamatwa,skanka kilogram 1,500,6 methamphetamine kilogram 687.76 heroin kilogram 19,20 na chupa 10 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina Fentanyl

Aidha Lyimo Amesema Tarehe 14 Novemba 2024 jijini dar es salaam Wilaya ya kigamboni mtaa wa Nyangwale, watuhumiwa Mohamed Suleiman Bakari (40) na sullesh said Mhailoh (36) wakazi wa Mabibo,Dar es salaam walikamatwa wakiwa na kilogram 1,350,4 za dawa za kulevya aina skanka,Dawa hizo zilifichwa ndani ya nyumba aliyopanga mtuhumiwa Mohammed, ambayo aliitumia kama ghala la kuhifadhi dawa hizo,dawa hizo zimepatikana Katika gari aina Nissan Juke yenye namba za usajili T 534 EJC,zikiwa tayari Kwa kusambazwa

Hata Hivyo Lyimo Ameongeza kuwa Katika mtaa wa pweza Sinza E, Wilaya ya ubungo jijini dar es salaam mtuhumiwa Iddy Mohammed Iddy (46) mkazi wa chanika Buyuni,alikamatwa akiwa na kilogram 150,2 za skanka,zilizokuwa zimefichwa Katika maboksi ya sabuni na baadhi ya dawa zikiwa zimefichwa kwenye boksi lililotengenezwa Kwa bati ngumu na kupachikwa kwenye chassis ya gari aina ya scania lenye namba za usajili wa afrika kusini LN87XJGP ambalo limekuwa likirumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Pia Novemba 17,2024 Katika Jiji la Tanga watuhumiwa Ally Kassim Ally (52) na Fahadi Ally Kassim (36) wamekamatwa mtaa wa mwakibila wakiwa na kilogram 706,96 za dawa aina ya heroin na methamphetamine,dawa hizo zimepatikana ndani ya gari aina ya Toyota Noah Yenye namba usajili T714 EGX na zengine zikibainika kufichwa kwenye nyumba aliyopanga mtuhumiwa

“Dawa zilizokamatwa ni nyingi na zingeweza kuwa na madhara makubwa Kwa jamii na taifa ikiwa zingeingia mitaani,Amesema dawa hizo haziathiri tu wale waliokwisha anza matumizi ya dawa za kulevya,Bali pia wanyabiashara Hawa hulenga watu wengine  ambao hawajaanza matumizi Ili kutanua masoko Yao,”Amesema Lyimo

Halikadhalika Mamlaka imebaini kuwa wahusika wa biashara haramu za dawa za kulevya hutumia mbinu ya kupanga nyumba ambazo zinageuzwa kuwa maghala ya kuhifadhi dawa za kulevya,huku wao wakiwa wakiishi Katika maeneo mengine

Aidha mamlaka inatoa Rai Kwa wamiliki wa nyumba kuwa Makini wanapopangisha vyumba zao,kwani nyumba inayotumika Kwa shughuli za dawa za kulevya ni kinyume Cha sheria na inaweza kutaifishwa,sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya,Sura ya 95 imeweka katazo Kwa mmiliki au Msimamizi wa nyumba, Msimamizi wa eneo au chombo Cha usafirishaji kuruhusu vitumike Kwa lengo la kutengeneza,kuvuta,kujidunga, kuuza au kununua dawa za kulevya

Lyimo amebainisha kuwa mmiliki anapojua kosa limetendeka kwenye eneo lake,anajukumu la kutoa taarifa Kwa mamlaka,kushindwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na akitiwa hatiani,adhabu yake inaweza kuwa faini kuanzia shilingi milioni Tano Hadi milioni Hamsini,au kifungu Cha miaka mitano Hadi miaka thelathini JELA au vyote Kwa pamoja.

About The Author

(Visited 8 times, 1 visits today)

Last modified: November 25, 2024

Close