Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira, amewahakikishia wananchi mkoani Mara kuwa Chama kitaendelea kuzibeba changamoto zinazowakabili na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi.
Miongoni mwa changamoto hizo ni ujenzi wa baadhi ya barabara ambazo zinapaswa kujengwa kwa lami ili kuzifungua baadhi ya wilaya za mkoa pia kuiunganisha Mara na nchi jirani ya Kenya kwa barabara za lami.
Wasira aliyasema hayo jana Rorya mkoani Mara alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Rorya,
“Sisi ni Chama Cha Mapinduzi, kazi yetu ni kusikiliza kero za watu, mnaweza tukacheza ngoma, lakini kama matatizo ya watu hayazungumzwi na hayatafutiwi ufumbuzi watu watakuwa hawana hakika kama Chama hiki kinashughulika na matatizo yao.
“Sasa nimemuelewa rafikiangu wa TANROADS tatizo lake la bajeti, anapewa sh. bilioni moja, kwa hiyo kama anatengeneza sana ni kilometa moja au moja na robo, na kwa kuwa barabara ina kilometa 56 maana yake ataikamilisha kwa miaka 56.
“Hilo ni tatizo la kibajeti ambalo inabidi kulifikisha kwa waziri anayehusika ili aone namna anavyoweza kusaidia kwa sababu jambo hili limeahidiwa na marais watatu” alisema.
Wasira alilazimika kueleza hayo baada ya Mbunge wa Rorya (CCM) Jafari Chege kueleza kuwa miongoni mwa changamoto za jimbo hilo ni baadhi ya barabara kutokuwa za kiwango cha lami.
Kwa mujibu wa Wasira, changamoto za wananchi lazima zifikishwe katika mamlaka husika “tutazungumza na mamlaka zinazohusika.”
“Mjue ya kwamba masuala haya ya maendeleo ni ya nchi yote siyo ya mkoa mmoja, kwa hiyo kama hatuwezi kwenda kusema yanayotusibu basi tutabaki hapa miaka 56 bila ya barabara, kwa hiyo tutafikisha hiyo hoja kwa waziri wa ujenzi na kwa sababu tumeshamweleza tutakwenda kusisitiza.
Barabara ziko nne katika mkoa wa Mara ambazo kwa bahati mbaya zote bado hazijakamilika kuna barabara inayokwenda Kilongwe, kuna barabara ya Tarime kwenda Serengeti, kunabarabara ya kutoka Sanzati-Nata-Mugumu na tuna barabara inayotoka Musoma kwesigasi.
Barabara zote zote hizo zipo katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa hiyo hatuendi kuzungumza jambo jipya, tunaenda kuhimizana namna ya kutekeleza Ilani ya Chama kwa sababu zipo katika Ilani ambayo inakamilika mwaka huu, hata kama hatutazimaliza tutakwenda kuingiza katika Ilani lakini utekelezaji uonekane unaendelea.
MBUNGE
Awali Chege akizungumza katika mkutano huo alimuomba Wasira kufikisha kilio cha wana Rorya cha kukosa barabara ya lami inayoliunganisha jimbo hilo na jirani ya Kenya.
“Uliuniuliza Chege nini Kinakusumbua nikakwambia cha kwanza ni barabara ya lami inayotoka Utegi, Shilati kwenda Kilongwe, umepita umeiona mwenyewe, barabara kwetu ni changamoto watu wa Rorya tunaomba barabara hii kwa kuwa ni ,uhimu kwa uchumi wa wananchi wa Rorya,”
About The Author
Last modified: February 8, 2025