Kutokana na Wizara ya Afya kuweka jitihada kubwa za uelimishaji jinsi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na usambazaji wa dawa za kutibu maji katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, wananchi kutoka Kijiji cha Jorodom wamevutiwa na jitihada hizo huku wakiomba dawa za kutibu maji ziongezwe zaidi .
Wakizungumza kijijini hapo akiwemo mwenyekiti wa Kijiji hicho wamesema hatua ya serikali kusambaza mabango ya kuelimisha kuhusu kuzingatia kanuni za afya kujikinga na magonjwa pamoja na usambazaji wa mabango ni nzuri katika kuwajali wananchi wake.
“Hii elimu ni nzuri sana maana maana inatupa mwongozo tufanye nini pia kitendo cha kutibu maji mnajali usalama wetu tunataka vidonge zaidi na zaidi “amesema mmoja wa wananchi hao.
Ikumbukwe kuwa Jorodom ni Kijiji cha kwanza kuathiriwa na maji ya mafuriko yaliyoambatana na maporoko ya tope ,magogo na mawe hali iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya maji, nyumba na vitu mbalimbali.
About The Author
Last modified: December 13, 2023