Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabella Mkojera akimuuliza maswali ya uelewa wa magonjwa ya moyo mkazi wa Pemba aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba kwaajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Hospitali hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce akimweleza mkazi wa Pemba umuhimu wa kutumia dawa za moyo wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba.
Baadhi ya wananchi waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba wakisubiri kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali hiyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano.
About The Author
Last modified: June 20, 2023