Visit Sponsor

Written by 1:06 pm KITAIFA Views: 17

UWT KUWEKA HISTORIA ZANZIBAR, KUMPONGEZA DKT. MWINYI

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wanatarajia kwenda kufanyia vikao vyao vikuu Visiwani Zanzibar, vikiambatana na sherehe kubwa ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dkt. Hussein Ally Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu ya mafanikio katika uongozi wake.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliyofanyika makao makuu ya umoja huo, Lumumba, Dar es Salaam Oktoba 27, 2023 ambapo pamoja na hayo alibainisha kwamba kauli mbiu yao katika sherehe hizo ni “MIAKA MITATU YA MAFANIKIO, NEEMA ZIENDELEE”. 

“Ndugu zangu, kama nilivyotangulia kusema awali, uongozi wa ndugu Mary Pius Chatanda (Mwenyekiti UWT Taifa) ni uongozi ambao unatengeneza historia nyingi na nyingine inaenda kutengenezwa kuanzia tarehe 1 mpaka 4, vikao vikuu vinakwenda kufanyika katika visiwa vya karafuu, Zanzibar, tutafanya sekretalieti yetu Zanzibar, lakini pia kamati ya utekelezaji itakaa Zanzibar, pia kwa mara ya kwanza Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania Chama Cha Mapinduzi litaketi katika Visiwa vya Zanzibar,” alisema Jokate.

Aidha Katibu Mkuu huyo wa UWT alisema kuwa tarehe 19, 3, 2023 walifanya sherehe za kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uwanja vya Uhuru, Dar es Salaam na sasa kamati yao imeridhia sherehe kama hizo zihamie Zanzibar kwa ajili ya kumpongeza Dkt. Mwinyi ambaye ameifanya Zanziba kuwa ya ‘moto’ tangu alipoingia madarakani.

“Dkt. Mwinyinyi alipokuwa anafanya kampeni zake alisema “Yajayo yanafurahisha”, sisi tunasema “Neema ziendelee” kwakuwa tumeziona. Huko nyuma Zanzibar kulikuwa na high season na low season kwamba kuna kipindi ambacho watu wanakuwa wengi kule na kuna kipindi cha kupoa, lakini safari hii hakuna cha high season wala low season, vipindi vyote Zanzibar ni ya moto na hiyo ni chini ya Serikali ya Dkt. Hussein Ally Mwinyi.” Alisema Jokate.

Vilevile alisema kuwa wanachokifanya UWT pamoja na mambo mengine ni kuwapa moyo viongozi wao wakuu, kuwashauri na kupokea maelekezo pia kuelezea yale makubwa ambayo wamefanya, walianza hivyo na Rais Samia sasa wanaenda kuelezea ya Dkt. Mwinyi Zanzibar na kwamba anatumia fursa hiyo kuwaalika UWT wote kwenye visiwa vya karafuu, Zanzibar wakayasemee yote mazuri yaliyofanywa na Rais Mwinyi ambapo kilele cha yote hayo kitafanyika tarehe 4, 11, 2023 katika viwanja vya Maisara kuanzia saa 12 asubuhi, kikipambwa na wasanii mbalimbali akiwemo Zuchu.   

About The Author

(Visited 17 times, 1 visits today)

Last modified: October 27, 2023

Close