Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameupongeza uongozi wa klabu ya Namungo kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya Uwanja wa Majaliwa ambao ni kichocheo cha uchumi na kitalu cha kukuza vipaji vya wanamichezo mkoa wa Lindi.
Waziri Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipotembelea kambi ya klabu ya Namungo na kuzungumza na viongozi na wachezaji wa Timu hiyo.
Uwanja huo umekuwa chanzo cha kukuza vipaji kwa vijana ambao wanajiunga na vilabu vingine na ambapo pia huchezea timu ya Taifa na kutoa mchango wao katika kupeperusha vyema bendera ya taifa kimataifa.
Klabu ya Namungo inakua ya kwanza kutembelewa na Mhe. Ndumbaro tangu alipoteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.
About The Author
Last modified: September 11, 2023