Visit Sponsor

Written by 3:47 pm MICHEZO Views: 7

UVCMM KAIRUKI JAMBO TULILOFANYA NIKUWAKUMBUSHA VIJANA MEMA YA MUUNGANO WETU



_UVCCM KAIRUKI_

TANZANIA ifikapo kila Aprili 26 ,inaadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964 na Aprili 28 mwaka 2025 vijana wa umoja wa Chama Cha Mapinduzi kutoka chuo cha Kairuki Jijini Dar es Salaam wameikumbuka siku hiyo kipekee kwa kuandaa Bonanza maalum lililohusisha Vijana wa Tanzania Bara na Visiwani


Akizungumza na waandishi wa Habari  Mgeni rasmi wa Bonanza hilo Ndg .Ayoub Dafa ambae ni mjumbe wa wilaya UVCCM Kinondoni ameanza kwa kuwapongeza Vijana hao kwa uzalendo na kusema wanachokifanya ni kuezi kazi zilizotukuka za Marais wote ambao ni  Dkt .Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt.Hussein Ali Mwinyi wa  ,Zanzibar




Nae Katibu wa umoja wa Vijana UVCCM Chuo cha Kairuki ambae ndie muandaji mkuu amesema wamefanikiwa kuandaa tukio hilo mahsusi la Muungano ili waadhimishe siku ya Muungano na kutoa shukrani kwa Marais wote waliyoyafanya kwa Vijana ikiwemo suala la Kuilinda Amani ,Kuwakumbuka vijana katika fursa mbalimbali na Suala la mikopo kwa vijana waliopo vyuoni kote bara na visiwani



Hatahivyo mgeni rasmi ametoa rai kwa vijana kwa  kuwakumbusha waendelee kuilinda amani ya Tanzania na waepuke kutumika vibaya kwakuwa wao wanabeba mustakabali wa Taifa letu



Mechi hiyo ilimalizika kwa Timu bara kushinda kwa Penati 4 – 3 Dhidi ya Team Visiwani mabao upande wa bara ndani ya dakika Tisini yalipachikwa na Ali Dakika ya 15 na 30 na upande wa Visiwani  yalifungwa  na Zaki 10 pamoja na Yusuf Dakika 50 hivyo mchezo ndani ya Dakika 90 kumalizika 2-2 kitendo kilichopelekea waende mikwaju ya Penati

About The Author

(Visited 7 times, 7 visits today)

Last modified: April 28, 2025

Close