Visit Sponsor

Written by 12:08 pm KITAIFA Views: 205

UTEUZI MPYA WA RAIS SAMIA HUU HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi kama ifuatavyo:
a) Uteuzi wa Katibu Mkuu
Amemteua Balozi Stephen Patrick Mbundi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia
masuala ya Afrika Mashariki. Balozi Mbundi atachukua nafasi ya Balozi Prof.
Kennedy Godfrey Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali.
b) Uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu
Amemteua Balozi Said Shaib Mussa – Balozi wa Tanzania, Kuwait kuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki. Balozi Mussa anachukua nafasi ya Balozi Fatma Rajab ambaye
ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, Oman.
c) Uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Amemteua Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn kuwa Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali. Balozi Prof. Gastorn anachukua nafasi ya Dkt. Evaristo
Longopa ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
d) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani
i) Amemteua Mhe. Jaji Lameck Michael Mlacha kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani. Kabla ya uteuzi Jaji Mlacha alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu,
Kigoma.
ii) Amemteua Mhe. Jaji Paul Joel Ngwembe kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi Jaji Ngwembe alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu,
Morogoro.
iii) Amemteua Jaji Mustafa Kambona Ismail kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi Jaji Ismail alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Divisheni ya
Rushwa na Uhujumu, Dar es Salaam.

iv) Amemteua Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi Jaji Issa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Zanzibar.
e) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu
i) Amemteua Dkt. Evaristo Longopa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya
uteuzi Dkt. Longopa alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
ii) Amemteua Bw. Wilbert Martin Chuma kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla
ya uteuzi Bw. Chuma alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufani Dar
es Salaam.
iii) Amemteua Bi. Sharmillah Said Sarwat kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bi. Sarwat alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Dar es Salaam.
iv) Amemteua Bw. Arnold John Kirekiano kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Kirekiano alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
v) Amemteua Bi. Martha Boniface Mpaze kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bi. Mpaze alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Jumuishi
katika Masuala ya Mirathi na Familia, Dar es Salaam.
vi) Amemteua Bw. Ferdinand Hilali Kiwonde kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Kiwonde alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.
vii) Amemteua Bw. Said Rashid Ding’ohi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla
ya uteuzi Bw. Ding’ohi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Iringa.
viii) Amemteua Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Dkt. Rumisha alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Dar es Salaam.
ix) Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
x) Amemteua Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Mwakahesya alikuwa Naibu Karani wa Baraza la
Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu, Dodoma.
xi) Amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Mwakapeje alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya
Kurekebisha Sheria, Wizara ya Katiba na Sheria, Dodoma.
xii) Amemteua Dkt. Dafina Daniel Ndumbaro kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Dkt. Ndumbaro alikuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dodoma.

xiii) Amemteua Bw. Emmanuel Ludovick Kawishe kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu. Kabla ya uteuzi Bw. Kawishe alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za
Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.
xiv) Amemteua Bw. Abdallah Halfan Gonzi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Gonzi alikuwa Mjumbe wa Baraza la Rufani za Kodi
(TRAT) na Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
xv) Amemteua Bw. Kamazima Kafanabo Idd kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Idd alikuwa Mhadhiri Msaidizi Chuo cha usimamizi wa
Fedha (IFM), Dar es Salaam.
xvi) Amemteua Bw. Frank Muyoba Mirindo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Mirindo alikuwa Mhadhiri Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto (IJA), Tanga.
xvii) Amemteua Bi Hadija Ally Kinyaka kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya
uteuzi Bi. Kinyaka alikuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili ya
Lawhill Co. & Advocates, Dar es Salaam.
xviii) Amemteua Bi. Aisha Ally Sinda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya
uteuzi Bi. Sinda alikuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili
BOWMANS Tanzania, Dar es Salaam.
xix) Amemteua Bw. Hussein Salum Mtembwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Bw. Mtembwa alikuwa Wakili wa Kujitegemea na Mmiliki
wa Kampuni ya Uwakili ya HM Noble Attorneys, Mtwara.
xx) Amemteua Bi. Irene Daniel Musokwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla
ya uteuzi Bi. Musokwa alikuwa Wakili wa Kujitegemea na Mshiriki katika
Kampuni ya Uwakili ya FC Attorneys, Dar es Salaam.

Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 03 Septemba, 2023.

About The Author

(Visited 205 times, 1 visits today)

Last modified: September 4, 2023

Close