Na. Beatrice Kaiza
Uanzishwaji wa viwanda vya magari waanza Rasmi nchini Tanzania kutoka Ghana huku ghana ikiwa na lengo kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ghana katika kundeleza uchumi na fursa mbalimbali.
Hayo Yamesemwa Jijini Dar es salaam na ofisa mkuu wa biashara kutoka wizara ya viwanda na biashara nchini Ghana. koffi odo akimuwakilisha waziri wa wizara hiyo ya viwanda kobina Hammond. Mara baada ya kuzindua maonyesho ya biashara yanaoyoendelea kufanyika ambayo maonesho hayo yanafahamika kwa jina la GHana expo 2024.
Kutokana na mazingira. Ambayo tumakutananayo Tanzania sisi kama waghana tunaenda kuanzisha mazingira Rafiki kwa waafrika ambayo ni hayafanani na mengineyo. Hivyo tunazingatia ubora katika utengenezaji wa magari hayo ili kwenda kupata masoko ambayo yanauzika kwa wananchi.

Aidha Oddo Amesema kuwa lengo la Maonyesho hayo ni kuweza kutambulisha bidhaa kutoka nchini Ghana kwani soko la Tanzania linaenda kuongeza tija ya biashara baina ya nchi hizo mbili hivyo wafanyabiashara kutoka Ghana na Tanzania wanaenda kufanya kazi kwa kushirikiana “Amesema Oddo
“Ushirikiano huo unaenda kuleta ushirikiano kwa Wantanzania kutoka Ghana na kwenda kupelekea Taasisi binafsi kuweza kushiriki kikamilifu kwenye AFCTA.
Kwa upande wake Balozi kutoka ghana katika mataifa ya Afrika mashariki William Abochi amesema kuwa wafanyabiashara kutoka nchini ghana imekuja ili kuchukua ujuzi mbalimbali kutoka sekta ya viwanda.
Ushirikiano katika biashara ni muhimu kwani wafanyabiashara wanapokutana hupeana mawazo tofauti tofauti na kuwezesha kutumia fursa ya kibiashara na uchumi wa biashara.
Sanjari na hayo meneja kutoka usimamizi na ukuzaji wa biashara kutoka mamlaka ya maendeleo Tanzania Tan trade ndug Mohamedi Tajiri akimuwakilisha mkurugenzi mkuu amesema kuwa sisi kama Tantrade tunafurahi kuona biashara mbalimbali zinafanyika katika kukuza uchumi wa nchi.
Kupitia maonyesho haya ya Ghana Expo 2024 tumeweza kupata fursa kuona wafanyabiashara mbalimbali wankuja nchini kuwekeza na kubadilishana mawazo,na biashara huku tukiendelea kujenga muktadha wa kuendeleza uchumi ambapo tunaenda kupata bidhaa kutoka Ghana ambapo tulikuwa tunazikosa na kuzipata za kwetu kwa kupitia Taasisi ambazo zimeweza kushiriki maonyesho hayo.
About The Author
Last modified: January 26, 2024