Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Katibu wa NEC – Itikadi, Siasa, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amesema kuwa vitendo vya vurugu wakati wa uchaguzi havikuwalenga viongozi wa upinzani pekee, bali hata makada wa CCM walijeruhiwa na kuuawa.
Akizungumza na wanahabari katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, Makalla amewataka Watanzania kulaani vitendo hivi kwa pamoja bila kupendelea upande wowote. Pia ameeleza kuwa dhana ya demokrasia haipaswi kuhusishwa na kushindwa kwa CCM pekee.
Aidha, Makalla ameonyesha kuwa migogoro ya vyama vya upinzani ni miongoni mwa sababu za ushindi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Alitoa shukrani kwa Watanzania kwa kuiamini CCM na kuipa ushindi mkubwa, akisema matokeo hayo ni ishara ya uungwaji mkono wa chama hicho.
About The Author
Last modified: November 29, 2024