Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Mtandao wa Haki ya Afya ya uzazi nchini Tanzania unaoongozwa na Doris Mollel Foundation na Chama cha wafanyakazi wa serikali na Afya Tanzania (TUGHE), wamepongeza hatua ya serikali na Bunge la Tanzania kuridhia na kupitisha marekebisho ya sheria, kwa kuongeza likizo kwa wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti, Wakisema hatua hiyo itasaidia kulinda ustawi wa Wafanyakazi.
Dkt. Jane Madete, Makamu Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Kwenye Hospitali ya Shre Hindumandal, Jijini Dar es salaam amewaambiwa wanahabari leo Jumatatu Februari 03, 2025 kuwa Maombi ya nyongeza ya muda wa likizo kwa Wafanyakazi Wanawake wanaojifunguaย watoto njiti yalianzishwa na kuasisiwa na Doris Mollel Foundation tangu mwaka 2017 na baadae mwaka 2023 kuungana
Mtandao wa haki ya Afya ya uzazi pamoja na TUGHE ambapo sasa kulingana na sheria hiyo mpya, Mfanyakazi atakayejifungua mtoto njiti likizo yake itaanza baada ya kufikisha wiki 40 za ujauzito na Baba wa mtoto njiti aliyezaliwa atapewa siku 7 za mapumziko.
Dkt. Madete amewaambia wanahabari kuwa Wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali ikiwemo za kiafya, hivyo wanahitaji muda mwingi wa kupumzika na kumuhudumia mtoto lakini pia wengi wamekuwa kwenye hatari ya kupoteza ajira zao jambo ambalo linaweza kupelekea msongo wa mawazo na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa malezi ya mtoto anayezaliwa.
TUGHE kwa kushirikiana na TUCTA na wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi ya Doris Mollel Foundation wanasema kufuatia nyongeza ya siku hizo za likizo itasaidia wanawake hao wanaokutana na changamoto kupata muda wa kutosha kuhudumia mtoto/ watoto na pia kuimarisha afya yake katika kipindi chote cha likizo na pasipo kuwa na wasiwasi wa kupoteza ajira sambamba na kumuweka mama katika afya imara.
Bungeni Dodoma, Januari 31, 2025, Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde kwa niaba ya Waziri Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu akielezea kuhysy mswada wa Marekebishi ya sheria za kazi wa mwaja 2024 alieleza kuwa kuanzia sasa mfanyakazi atakayejifungua mtoto njiti likizo yake baada ya kufikisha wiki 40 za ujauzito na baba wa mtoto njiti atakayezaliwa atapewa siku saba za mapumziko.
About The Author
Last modified: February 4, 2025