Visit Sponsor

Written by 3:00 pm KITAIFA Views: 30

TPA YAKANUSHA KUWEPO KWA TAARIFA YA KUKWAMA KWA SUKARI BANDARINI

Na Beatrice Kaiza

Mkurugenzi Wa Bandari Ya Dar es Salaam Mrisho Mrisho amekanusha na kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizosambaa kuwa ipo sukari iliyokwama Bandarini na kuleta taharuki kubwa Nchini

Mrisho amesema kuwa zipo meli zilizoleta sukari nchini na tayari sukari imeshashushwa na tayari kwa kuwahudumia wananchi.

Ndani ya Mwezi Januari pekee Bandari ya Dares Salaam imehudumia takribani ya
Meli zipatazo 86 pamoja na kuwepo kwa hali ya mvua kubwa lakini shughuli za kiuendeshaii katika Bandari ya Dares Salaam zimeendelea kufanyika vyema huku gati zote ndani va bandari hivo zikiendelea na shughuli za kupakia na kupakua mizigo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Februari 04, 2024 na Mkurugenzi wa Bandari ya Dares Salaam Bw. Mrisho Mrisho wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya uwepo wa msongamano bandarini.

Mrisho amethibitisha kuwa gati zote zinaendelea kufanya kazi kama kawaida na kwa sasa Meli zinaendelea kuhudumiwa katika gati zote.

About The Author

(Visited 30 times, 1 visits today)

Last modified: February 5, 2024

Close