Visit Sponsor

Written by 11:26 am KITAIFA Views: 6

TASAC YANG’ARA TUZO ZA UANDAAJI WA TAARIFA YA MAHESABU KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, CPA Benjamin Mashauri (kulia) ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mkurugenzi wa Fedha, CPA Pascal Kalomba (kushoto), tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa viwango vya kimataifa kwa mwaka 2023. TASAC imeshika nafasi ya kwanza kati ya Mamlaka 9 za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius Maneno

DAR ES SALAAM


Na Mwandishi Wetu,


Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeshika nafasi ya kwanza katika tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa mwaka 2023 kati ya Mamlaka 9 za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini.

Tuzo hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, CPA Benjamin Mashauri ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Novemba, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha, CPA Pascal Kalomba kwa  niaba ya Mkurugenzi Mkuu  wa TASAC, Bw. Mohamed Salum.

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hiyo, CPA Mashauri, alisisitiza umuhimu wa taasisi za umma kuzingatia viwango vya kimataifa katika uandaaji wa taarifa za kifedha ili kuboresha utawala bora.

Kwa upande wake, CPA Kalomba, alisema mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja za wafanyakazi wa shirika hilo.
“Hii inaonesha dhamira yetu ya kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinasimamiwa kwa uwazi, uwajibikaji, na ufanisi,” alisema.

TASAC imeshika nafasi ya kwanza kwa mara ya tatu mfululizo, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2021, mara pili mwaka 2022 na mara tatu kwa mwaka 2023.
Kwa mwaka 2023, jumla ya taasisi 86 za Serikali na sekta binafsi katika maeneo wanayothibiti zimeshindishwa.


About The Author

(Visited 6 times, 1 visits today)

Last modified: December 1, 2024

Close