Visit Sponsor

Written by 1:10 pm KITAIFA Views: 14

TARURA  YAENDELEA NA UJENZI  WA MITARO MIKUBWA YA MAJI MKOANI  TABORA

#Wananchi watakiwa kutunza na kusafisha mitaro ya maji

Tabora

Wakala ya Barbara  za Vijijini na Mijini (TARURA ) mkoani TABORA unatekeleza ujenzi wa mitaro mikubwa  ya maji ili kuondoa kero kwa wananchi hasa kipindi cha masika ambapo maji yamekuwa yakiingia kwenye  makazi ya watu.

Akiongea wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi mkoani hapa, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI  anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila ameitaka TARURA  kuhakikisha mitaro hiyo inafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

“Kuna haja  ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara na kufanya usafi katika mitaro hii ili maji yapite kwa urahisi na kuondoa kero kwa wananchi kama ilivyokusudiwa”.Amesema Mhandis Mativila.

Hata hivyo Mhandisi Matavila amewataka viongozi wa Manispaa na TARURA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutunza na kusafisha mitaro hiyo ili kuepuka mafuriko na magonjwa ya mlipuko.

Aidha,amewasihi wananchi wanaoishi karibu na mitaro hiyo kujitolea kwa hali na mali ili kuisafisha mitaro hiyo badala ya kukaa na kuisubiri serikali pekee.

Naye, Meneja wa TARURA  Wilaya ya TABORA  Mhandisi  Subira Manyama amesema kuwa  hadi sasa wamejenga mitaro yenye urefu mita 158 ambayo imesaidia wananchi kwa kiasi kikubwa.

“Kulikuwa na kero ya maji kuingia kwenye  makazi ya watu lakini sasa kero hiyo imeondolewa ambapo mpango uliopo ni kuhakikisha tunaondoa kabisa mafuriko kwa kujenga mitaro yenye urefu wa km 25”.

(Visited 14 times, 1 visits today)

Last modified: June 11, 2024

Close