Visit Sponsor

Written by 12:03 pm MICHEZO Views: 89

TANZANIA YAPOKEA OMBI LA PALESTINA KUANZISHA KITUO CHA MICHEZO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Tanzania Mhe. Hamdi Mansour Abuali  Oktoba 19, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Mhe. Ndumbaro amepokea maombi ya nchi ya Palestina kupitia Balozi huyo, kuanzisha Kituo cha Michezo Jijini Dar es Salaam nakuahidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Mhe. Balozi  Hamdi amewasilisha Ombi hilo akieleza kuwa nchi hiyo ina ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo Utamaduni na Michezo, hivyo Kituo hicho kitakua na umuhimu kwa nchi mbili hizo katika kukuza michezo.

About The Author

(Visited 89 times, 1 visits today)

Last modified: October 19, 2023

Close