Visit Sponsor

Written by 3:43 pm KITAIFA Views: 11

TANZANIA YAJIZATITI KATIKA MIFUMO YA KIDIGITALI YAWAPIKU MATAIFA MENGINE

Na Madina Mohammed DAR ES SALAA MWANAHABARI

Waziri wa habari mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe Jerry Silaa amefungua kikao kazi Cha siku tatu ambacho kimejikita kufanya mapitio Katika maeneo 11 ambayo nchi za Afrika zilijiwekea awali Katika mkutano wa Dunia wa jumuiya ya habari WSIS

MHE waziri amefungua kikao hicho Leo Tarehe 09 Oktoba 2024 Katika kituo Cha mikutano Cha kimataifa Cha Julius Nyerere JNICC jijini dar es salaam

Kikao hicho kazi kinatarajiwa kufikia tamati Oktoba 11,2024 kimeandaliwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na kamisheni ya umoja wa mataifa UN Kuhusu UCHUMI wa nchi ECA

Aidha Kupitia kikao hicho ambacho kimewaleta pamoja watunga sera, wataalamu na wadau kutoka Afrika na nje ya Afrika kinafanya tathimini ya mafanikio na mapungufu Katika utekelezaji wa mkakati waliojiwekea Katika miongo miwili iliyopita na kuimarisha ushirikiano na Kujenga jamii ya kidigitali shiriki na endelevu

UNECA ambayo inayoshughulika na masuala ya ICT,miaka 20 iliyopita mwaka 2003 Geneva na mwaka 2005 Tunis kulifanyika mkutano unaoitwa WSIS Ambapo mwakani itakuwa ni WSIS+ 20 ambayo ni miaka 20 baada ya mkutano huo

Mkutano huo uliweka action 11 Kwa ajili ya kuwezesha ama nchi za Afrika ziweze kujipanga kwenye masuala ya kidigitali

“Kikao hichi kazi kimekuja kufanya mapitio ya kuona Yale maeneo 11 ambayo nchi za Afrika zilijiwekea wamefikia wapi, wanachangamoto Gani,kunayapi ya kujifunza Kwa ajili ya kuelekea mkutano wa mwakani” Amesema Silaa

Kwa mujibu wa Silaa Amesema miongoni mwa maeneo hayo ni upatikanaji wa taarifa na maarifa Kwa wote kuanzia ngazi ya kitaifa Hadi kimataifa

Pia eneo lingine likiwa ni kuimiza na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali,sekta binafsi na jamii Ili kufikia mawasiliano jumuishi na endelevu

Vilevile Katika mkutano huo walikubaliana kuhusu Kuendeleza miundombinu ya Teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA Ili kuhakikisha hakuna kundi ambalo linaachwa nyuma

Jambo lingine ni Kuhusu wa Kujenga ujuzi na uwezo wa kutumia Teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA

“Na Katika nchi hizi za Afrika Tanzania imeibuka namba Moja Kwa hiyo na si.tu kwenye masuala ya uwekezaji wa TUME ya TEHAMA na miundombinu Kwa maana connectivity na coverage lakini vile vile hata Kwa kiutendaji tuko vizuri”.

Pia,Amesema kikao kazi hicho kimekuja ikiwa wiki ijayo kongamano la kihistoria la TEHAMA linatarajiwa kufanyika hapa Nchini

Nae mkuu wa idara ya ubunifu na Teknolojia wa kamisheni wa umoja wa mataifa UN Kuhusu uchumi wa Afrika ECA Dkt Mactar Seck Amesema maeneo hayo 11 watayafanyia mapitio ya kina Ili kuja na yatokanayo ambayo ni muhimu Kwa mkutano ujao wa WSIS+ 20

Amesema matokeo ya kikao kazi hiki Cha siku 3 yataandaliwa ripoti ya kina ya mapitio itakayotoa mapendekezo ya sera Kwa jamii ya kuongeza utekelezaji wa WSIS barani Afrika

About The Author

(Visited 11 times, 1 visits today)

Last modified: October 9, 2024

Close