Visit Sponsor

Written by 12:14 pm KITAIFA Views: 30

TANZANIA NA INDIA KUKUZA UHUSIANO KIMKAKATI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiwa kwenye picha na Rais wa India Mhe. Droupadi Murmu pamoja na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo tarehe 09 Oktoba, 2023

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na India zimekubaliana kukuza
uhusiano wao wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili kwa kiwango cha Ushirika
wa Kimkakati.
Rais Samia ameyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika
ziara yake ya kitaifa ya siku 3 nchini India.
Miongoni mwa masuala ambayo viongozi hao wameyawekea msisitizo katika
ushirikiano ni pamoja na ulinzi, nishati, kujenga uwezo, usalama wa majini, biashara
na uwekezaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa KitaifaHyderabad House New Delhi Nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.


Hadi kufika mwaka 2022, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili ulifikia dola za
Kimarekani bilioni 3.1, hivyo kuifanya India kuwa mshirika wa tatu kwa ukubwa
katika biashara na mwekezaji wa tano kwa ukubwa nchini Tanzania.
Wakati huo huo, nchi hizo mbili zimetia saini hati za makubaliano 14 na mkataba
mmoja, ambapo hati 10 zimehusisha taasisi za serikali na mitano ni za sekta binafsi.
Mbali na kuwa tayari India inaisaidia Tanzania katika masuala ya ubobezi wa
kupandikiza figo na uboho (bone marrow), pia viongozi hao wamejadili namna ya
kuanzisha kituo cha dawa asilia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakijibuswalilililoulizwa na waandishi kuhusu mategemeo ya ziara yake nchini India tarehe 09 Oktoba, 2023.


Rais Samia ameshukuru pia kwa kuanzishwa kampasi ya kwanza ya chuo cha IIT
nje ya India chenye hadhi ya juu katika masuala ya teknolojia visiwani Zanzibar
kitakachowanufaisha wanafunzi mbalimbali, siyo tu wa Tanzania ila hata nje ya
mipaka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima wakati wa hafla ya mapokezi yake katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo tarehe 09 Oktoba, 2023.


Masuala mengine yaliojadiliwa katika ziara ya Rais Samia ni pamoja na usalama wa
mitandao, kushirikisha vijana hasa kupitia vyuo vya VETA, kutoa mafunzo kwa
wahandisi wa madini, kushirikiana kwenye kilimo na miradi ya maji.

About The Author

(Visited 30 times, 1 visits today)

Last modified: October 9, 2023

Close