Visit Sponsor

Written by 2:08 pm KITAIFA Views: 32

TAASISI UHISANI ZAOMBWA KUONGEZA NGUVU UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA JAMII

Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman akiwa zawadi maalum leo kutoka Mtandao wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPN) wakati wa tukio la ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPC), ambao umeratibiwa na EAPN kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF) pamoja na wanachama wengine.

Wito huo umetolewa leo Jumatano, visiwani Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, akifungua mkutano wa nane wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPC), ulioandaliwa na Mtandao wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPN), kwa kushirikiana na Kituo cha Huduma za Kisheria (LSF).

Othman amehimiza taasisi hizo kuimarisha umoja na nguvu katika kukabiliana na changamoto zinazohitaji juhudi za pamoja kuzitatua, ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini, ukosefu wa usawa na athari zilizotokana na janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).

Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman akitoa hotuba ya ufunguzi leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPC), ambao umeratibiwa na Mtandao wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPN) kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF) pamoja na wanachama wengine.

“Mabadiuliko ya mifumo yenye athari yanahitaji mbinu ya kina na jumuishi ambao inavuka mipaka ya jiografia, itikadi na sekta. Ni kupitia ushirikiano thabiti wa ndani, kikanda na kimataifa ndipo tunaweza kutumia nguvu kubwa ya hatua za pamoja ili kukabiliana na changamotoi nyingi mbele yetu,” amesema Othman.

Aidha, Othamna amesema kauli mbiu ya mkutano huo ya “Mabadiliko ya mifumo: kuchochea hatua za pamoja” inaunga mkono dhamira ya Zanzibar katika kukabiliana na changamoto za kimfumo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akitoa neno neno fupi la ufunguzi leo wakati wa Mkutano wa Nane wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPC), ambao umeratibiwa na Mtandao wa Uhisani Afrika Mashariki (EAPN) kwa kushirikiana na LSF pamoja na wanachama wengine.

“Tunabaki katika harakati zetu za kufungua uwezo uliofichika ndani ya mifumo yetu ili kuunda jamii ambayo sio tu yenye ustawi na endelevu, bali pia jumuishi kwa uthabiti

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, amesema nguvu ya taasisi za uhisani Afrika, imeelekezwa katika kuwezesha jumuiya zenye maendeleo endelevu, ambapo zimekuwa zikitoa rasilimali, utaalamu na mitandao ili kukuza mabadiliko ya kudumu.

Lulu amesema mkutano huo wa siku tatu, kuanzia leo tarehe 28 hadi 30 Juni 2023, unalenga kuangalia namna ya kuongeza juhudi za ushirikiano wa taasisi za uhisani ili kukuza mazingira yanayofaa kwa ukuaji wa uhisani barani Afrika.

“Sisi LSF, tunapenda kusikia mitazamo yote na tunaamini kwa uthabiti majadiliano katika jukwaa hili , yanaweza kuwa hatua nyingine muhimu kuelekea mabadiliko ya mifumo kote na kwa hivyo, kuongoza juhudi za maendeleo endelevu. Nawatakia mapumziko mema Zanzibar,” amesema Lulu.

About The Author

(Visited 32 times, 1 visits today)

Last modified: June 28, 2023

Close