Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere,amewaomba wanasiasa nchini kuachana na kuzihusisha timu za Simba na Yanga kwenye mambo ya siasa kwani kufanya hivyo kutaleta migogoro kwenye mpira.
Pia mwenyekiti huyo amewataka baadhi viongozi wa dini nchini kuacha tabia ya kutumia siasa kwenye Nyumba za Dini.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar,Nyerere,amesema kumeibuka baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakizitumia timu hizi kongwe kwenye siasa.
“Hizi ni timu kongwe zimeanzishwa kabla hata mimi sijazaliwa,sasa unakuta mwanasiasa anakwambia ningekuwa Rais wa nchi hii ningezifuta Simba na Yanga,yaani wameshaanza kuziingiza kwenye siasa jambo ambalo sio zuri”amesema Nyerere.
Akizungumzia upande wa Viongozi wa Dini,Nyerere amesema wapo baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa matamko kwenye nyumba za ibada yenye lengo wa upande wa siasa.
Amesema jambo hilo ni hatari kwa Taifa linaweza kuligawa Taifa ambalo linasifika kwa amani.
“Sahivi kuna mmonyoko mkubwa wa maadili kwenye jamii,lakini nashangaa hawakemia haya mambo lakini nashangaa wanazungumzia siasa badala ya kukemea haya”Amesema
About The Author
Last modified: April 29, 2025