Visit Sponsor

Written by 12:43 pm BIASHARA Views: 5

SOKO LA KARIAKOO KUZINDULIWA RASMI BIASHARA SASA SAA 24

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amezindua ufanyaji Biashara Saa 24 katika soko la Kimataifa la Kariakoo.

Utoaji wa huduma za kibiashara kwa saa 24 unalenga kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuongeza mapato ya Serikali na kutoa fursa zaidi za ajira.

Ameyasema hayo hapo Jana 27 Frebuari 2025 wakati akizindua soko hilo la biashara la saa 24 la kimataifa la kariakoo na kufuatiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wasanii wa Bongo fleva’ na bongo movie

Chalamila Amesema BILIONI 28 zilitolewa na Mhe rais Samia Suluhu Hassan Kwa kukarabati upya soko hilo Kwa kulijenga upya soko hilo la kimataifa la kibiashara

“Kwa Tanzania vision imebebwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Dar es salaam ina vitu vyote vilivyopo mkoani lakini viongezi vipo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Mikoa mingi ina bandari lakini kwenye sifa Dar inaongezeka. Sisi hatuanzishi jambo jipya sana kufanya biashara usiku. Tunaanzisha jambo kwa kutembelea kwenye nature. Na nature inasema hospitali nyingi za Dar es Salaam zipo wazi. Mtu anayemuuguza mgonjwa anataendaje hospitali? Kwenye mnyororo huo huo utamuhitaji mtu wa daladala, pikipiki kufanya kazi”- Albert Chalamila, RC Dar es Salaam.

Aidha Amesema Soko hilo litaweza kufungwa Taa Zaidi ya 730 Kwa agizo hilo limetoka Kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Kwani anachoitaji tuwashe taa zikiwa ni juhudi za wafanyabiashara

“Wazo la wafanyabiashara kufanya biashara usiku ni wazo la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba tusaidiane na wafanyabiashara wa Mataifa wengine waje wapate service hapa Dar es Salaam. Wananchi wote wanaoongozwa na ndugu yetu Paul Kagame (Rwanda), Felix Tshisekedi, (Kongo) Lazarus Chakwera na wengine wengi sana waweze kuja hapa Dar es Salaam ili waweze kufanya biashara hizi ambazo zimekusudiwa”- Albert Chalamila, RC Dar es Salaam.

Chalamila amesema kuanzia wiki ijayo ataunda kamati maalumu ya kupitia upya sheria ndogondogo za Halmshauri zinazokinzana na watu kufanya biashara saa 24 ili kuona namna ya kuziondoa sheria hizo.

Aidha amesema atamshauri pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwakuhusu namna ya kuziondoa sheria hizo ili watu waweze kufanya biashara saa 24 kama ilivyozinduliwa Leo.

“Wananchi wote wanaoongozwa na ndugu yetu Paul Kagame (Rwanda), Felix Tshisekedi, (Kongo) Lazarus Chakwera na wengine wengi sana waweze kuja hapa Dar es Salaam ili waweze kufanya biashara hizi ambazo zimekusudiwa”- Albert Chalamila, RC Dar es Salaam.


Paul John Walalaze, Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi  Tanzania Amesema kuwa Kuna Kodi za aina mbalimbali, mapato hali hii iliyofanyika hapa ni kiashiria tosha kinachosema kwamba wananchi wanakwenda kupata mauzo makubwa kwenye biashara zao kama walipa kodi. Kuna lile agizo ambalo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwamba tukasajili wafanyabiashara, tukaongeze idadi ya Wafanyabiashara. Biashara zikiongezeka kama hivi itakuwa ni rahisi kuweka ushawishi kwa watu kusajili biashara


“Ukiona biashara zinafunguka, nchi inafunguka basi na sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA tunanyanyua masikio yetu maana yake kusikilizia matokeo ya kufunguka kwa biashara. TRA kuna indicators ambazo sisi tunaziangalia cha kwanza ni biashara kukua. Ukiona mauzo, manunuzi yanaongezeka na utoaji wa huduma unaongezeka tunategemea impact au matokeo yake ni kuongeza kwa ule mzunguko na kunaleta Kodi”- Paul John Walalaze, Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi  Tanzania

Mtume na Nabii Boniface Mwamposa (Buldoza) wa Kanisa la Arise and Shine, (Inuka Uangaze) Kawe Amesema kuwa Kufungua biashara Saa 24 ni ki- Biblia kabisa ni kimaandiko kabisa ni kimaandiko, hata Mungu mwenyewe wakati anaumba hakuna mahali ilisema alilala. Imeandikwa ikawa asubuhi, mchana na usiku. Na ukisoma vizuri maandiko Mungu anasema malango yako yatakuwa wazi usiku na mchana

“Kufungua biashara Saa 24 ni ki- Biblia kabisa ni kimaandiko kabisa ni kimaandiko, hata Mungu mwenyewe wakati anaumba hakuna mahali ilisema alilala. Imeandikwa ikawa asubuhi, mchana na usiku. Na ukisoma vizuri maandiko Mungu anasema malango yako yatakuwa wazi usiku na mchana”- Mtume na Nabii Boniface Mwamposa (Buldoza) wa Kanisa la Arise and Shine, (Inuka Uangaze)

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: February 28, 2025

Close