Visit Sponsor

Written by 4:13 pm KITAIFA Views: 8

SIMBACHAWENE AWATAKA VIONGOZI WA TAKUKURU KUBADILI CHANGAMOTO KUWA FURSA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamisha wa Polisi, Salum Hamduni akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene tuzo ya kuthamini mchango wake katika mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023 wa Viongozi wa Taasisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka Viongozi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutafakari
kwa kina na kujadili changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi na
kuzifanya kuwa fursa kwa maendeleo ya Taifa.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo tarehe 20 Novemba, 2023
wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa
TAKUKURU-2023 katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma.
“Ninaamini mtatumia fursa ya mkutano huu wa mwaka kujadili masuala
yote yanayoonekana kuwa ni changamoto katika utendaji kazi ili kupata
suluhu ya pamoja” ameongeza Mhe. Simbachawene.
Aidha, katika hotuba yake amebainisha kuwa kila mmoja katika
mazingira tofauti na kwa namna ya pekee ameruhusu au ameathiriwa na
rushwa, hivyo ametoa rai kwa wananchi wote kuhakikisha wanazuia
mianya ya rushwa ili kutoathiri vizazi vijavyo.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa TAKUKURU inatakiwa kuitumia
vizuri programu iliyoianzisha ya TAKUKURU Rafiki kwa lengo la
kupanua wigo na kuwashirikisha wananchi katika kupambana na
rushwa.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Salum
Hamduni amesema ofisi yake inaendelea na utekelezaji wa shughuli
zake kwa mujibu wa Sheria na sasa wamejikita zaidi katika kuzuia
rushwa.
“Tunaendelea na kazi ya kuelimisha umma kuhusu masuala ya rushwa
na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Serikali ambapo tumeokoa fedha
nyingi ambazo kama isingekuwa TAKUKURU basi fedha hizo zingeishia
mikononi mwa watu binafsi” amesema Bw. Hamduni.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU hufanyika kila
mwaka kwa lengo la kubainisha changamoto zinazowakabili katika
utendaji kazi wao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja. Mkutano huu wa

Mwaka kwa mwaka 2023 una kaulimbiu ya Kuzuia rushwa ni jukumu
lako na langu, tutimize wajibu wetu.

Kwa upande wake, mmoja wa washiriki wa mafunzo ya walimu mahiri
wanaofundisha darasa la awali Bi. Sophia Kilavi ameishukuru Serikali kwa
kuwapatia mafunzo ya maudhui ya mtaala mpya wa mwaka 2023
ulioboreshwa ambao wanakwenda kuutekeleza.
Bi. Kilavi amesema wamejifunza kwamba katika ufundisha wa watoto wa
elimu ya awali wanapaswa kutumia vifaa vya TEHAMA vikiwepo
vishikwambi, komputa na Televisheni ili kuwawezesha watoto kumudu
stadi mbalimbali zilizokusudiwa katika mtaala.
Aidha, Bi. Kilavi amesema pia wamejifunza namna ya uchopekaji wa
masuala ya mtambuka ikiwemo elimu ya fedha ya fedha ya kitanzania, utu,
maadili, imani na utamaduni.
Mafunzo haya kwa awamu ya kwanza yamewahusisha jumla ya walimu
1,832 ambao wamegawanyika katika vituo vitano ambavyo ni Chuo cha
Ualimu Kleruu na katika Shule za msingi Gangilonga, Kiesa, Kigambani, na
Njia Panda.

About The Author

(Visited 8 times, 1 visits today)

Last modified: November 20, 2023

Close