Visit Sponsor

Written by 12:08 pm KITAIFA Views: 39

SIMBACHAWENE ARIDHISHWA NA UJENZI OFISI ZA TAKUKURU NA TUME YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wakandarasi na watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. George Simbachawene amewasisitiza wakandarasi wanaojenga
majengo ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na
Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma kuendelea kufanya kazi kwa bidii na
kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mikataba.
Mhe. Simbachawene amesema hayo kwa nyakati tofauti leo tarehe 15
Novemba, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa majengo hayo jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Simbachawene amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kutoa fedha nyingi na kwa wakati kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi kwa
taasisi zilizo chini ya ofisi yake.
“Majengo haya yameanza kujengwa wakati Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
anaingia madarakani na kulikuwa na mtikisiko wa uchumi na majanga
mbalimbali duniani lakini hakusitisha kuleta fedha za ujenzi wa majengo
haya. Hivyo, hatuna budi kuendelea kumuombea dua na sala ili aendelee
kutuongoza kwa hekima na busara” amesema Mhe. Simbachawene.
Pia, amewapongeza TAKUKURU kwa ubunifu wa kulipa Mkandarasi kwa
mfumo wa milestone lengo likiwa ni kuimarisha mtiririko wa fedha kwa
mkandarasi kulingana na kazi inavyofanyika na kutoa fursa ya kukamilisha
jengo kwa wakati.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Salum
Hamduni amesema kwa kibali cha mamlaka ya bajeti, Mshitiri ameridhia
malipo ya mkandarasi yafanyike kwa kutumia utaratibu wa milestone badala
ya kutumia utaratibu wa vyeti vya malipo ya mpito (interim payment
certificates) ili kukamilisha mradi wa ujenzi ifikapo Julai, 2024.
Kamishna Hamduni ameongeza kuwa, mpango wa kutumia utaratibu wa
malipo kwa milestone utaanza tarehe 4 Disemba, 2023 na utatoa fursa kwa
mkandarasi kulipwa kiasi cha fedha kulingana na kazi alizopanga kuzifanya
na kuzikamilisha kwa asilimia 100.

2

Katika hatua nyingine, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya
Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Simbachawene amesema katika kipindi
cha miezi kumi (10) mkandarasi ambaye ni Kampuni ya CRJE (East Africa)
amefanya kazi kubwa, kwa haraka na ufanisi ya ujenzi wa ofisi hiyo.
“Ninawasisitiza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kusimamia kwa
ukamilifu ujenzi huu ili jengo likamilike kama linavyoonekana kwenye mchoro
wa jengo hili” amesema Mhe. Simbachawene.
Kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew
Kirama amesema ujenzi huo unajumuisha ujenzi wa jengo la sakafu sita (6),
nyumba ya mlinzi, chumba cha kuhifadhi mitambo ya umeme, kibanda cha
kukusanya taka, ujenzi wa uzio na utengenezaji wa mandhari ya nje ya jengo
ambapo hadi sasa mkandarasi amefikia asilimia 50 ya kazi zote.
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma ulianza terehe 12
Januari, 2023 na Mkadarasi akiwa ni Kampuni ya CRJE (East Africa) na kwa
mujibu wa mkataba anatakiwa kukabidhi jengo hilo ifikapo Septemba, 2024.

About The Author

(Visited 39 times, 1 visits today)

Last modified: November 16, 2023

Close