Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ametoa wito kwa wataalamu wa ndani kuchangamkia fursa zinazotokana na miradi mikubwa ya ujenzi nchini.
Akizungumza Wakati akimuwakilisha Naibu waziri mkuu na waziri Wa Nishati na Madini Doto Biteko katika Kongamano la Tano la Bodi ya Usajili wa Wakadiriaji Majenzi na Wahandisi jijini Dar es Salaam Oktoba 29, 2024, Mpogolo amesema ni muhimu kwa wataalamu wa ndani kutumia uwezo wao katika miradi ya serikali ili kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje.
Mpogolo amebainisha kuwa, ingawa wataalamu wa ndani wanakabiliwa na changamoto ya mitaji midogo, wanapaswa kuongeza juhudi zao kushiriki katika miradi hiyo badala ya kuruhusu serikali kutumia wataalamu wa nje, hali inayosababisha upotevu wa fedha za kigeni. Amehimiza wataalamu wa ndani kushirikiana kwa kuondoa ubaguzi katika utoaji wa fursa za kazi ili kufanikisha miradi hiyo kwa umoja.
Aidha, Mpogolo amekemea tabia ya baadhi ya wataalamu wa ndani kuwatafuta wataalamu wa nje na kushirikiana nao huku wao wakipata sehemu ndogo ya faida. Alisisitiza kuwa mshikamano na ushirikiano wa kitaifa ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya sekta ya ujenzi na kuimarisha uchumi wa nchi.
Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt Daudi Kondoro ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania( TBA) amesema kuwa watendaji wa Wizara wataendelea kusimamisha sekta ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ili waweze kua na weledi katika kazi zao.
“Wizara ya ujenzi itatenga fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo wataalamu 180 Kila Mwaka ambao wanahusika na bunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ili waweze kujengewa weledi zaidi na zaidi katika taaluma yao” amesema Dkt.Kondoro
Na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi wa wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Dkt Ludigija Bulamile amesema kuwa kwa sasa Bodi hiyo imesajili 1586 ambapo kati yao 33 ni wageni kutoka nje ya nchi hivyo shughuli zao wanazozifanya zinakwenda kwa kuzingatia weledi na wale wanaokosea wamekuwa wakiwaonya ili wasitie doa wazawa kutoaminika
Naye Miongoni mwa aliyetunukiwa cheti Mhandisi Alfayo Khamisi ameshukuru sana kufikia hatua hiyo hadi kupata cheti hivyo atajitahidi anakwenda kuwajibika katika shughulizake kwa weledi.
Kongamano hilo lililenga kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya ujenzi, pamoja na kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali.
About The Author
Last modified: October 29, 2024