Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Shilingi million Mia 100 kutumika kujengea hospital za zahanati Saranga
RAIS SAMIA Amenunua kifaa kinachouzwa Zaidi ya billion 30 ambacho kinachogundua kansa hatua ya kwanza
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila amewaomba wananchi kuisemea serikali Kwa mambo ambayo inayofanya Kwa utendaji wa miundombinu na miradi inayotekelezwa na serikali na sio kulalamikia serikali
Amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imejitaahidi Kwa namna Pana sana kuboresha sekta ya afya nchini na Mhe Rais amekuwa ni kinara mkubwa sana wa kuokoa maisha ya Mtoto na Mama mjamzito

Ameyasema hayo 9 April 2025 Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila Amesema Mkoa wa dar es salaam ni mkoa ambao unahudumia namna kuu mbili za watu unatoa huduma Kwa wakazi wa dar es salaam na ni mkoa unaotoa huduma nje ya mkoa wa dar es salaam
Amesema Sekta ya afya ukienda Muhimbili Mlogazila JKCI ocean road mhe rais amewekeza fedha nyingi Kwa wataalumu na vifaa Tiba ili wagonjwa wote waweze kupata huduma

“Katika ngazi kubwa ya kitaifa mhe.rais ameibeba sekta ya afya sawasawa na ndomana pale Mlogazila Kuna madaktari bingwa”Amesema Chalamila
Chalamila Ameongeza kuwa Mwaka Jana mhe.rais.amewalipia madaktari bingwa si chini ya 600 Ili waongeze uzoefu waje watibu Katika mahospital zetu makubwa ambayo Leo mumesikia kunahuduma za kupandikiza Figo kunahuduma ya kufanya operesheni bila ya kupasua kunahuduma ya kufanya operesheni ya ubongo bila ya kupasua hayo yanapatikana dar es salaam

“naungana na nyie watanzania wa saranga kwamba tuibebe ajenda hii ya kituo hichi kiweze pia kukamilika lakini pia nafahamu kituo hichi kitakuwa ni Kwa huduma za msingi tu zile za awali Wala hautafanyiwa upasuaji mkubwa hapa,kumuona daktar wa kibingwa tutakapokamilisha hiki zinakuwa zile huduma za kawaida alafu baada ya hapo utakapopewa rufaa mahospital makubwa utayaona na ndipo utakaposema Asante mungu na nijalie Samia Suluhu Kwa huduma hizi”Ameongeza chalamila

Amebainisha kuwa Wanadar es salaam pamoja na vilio wanavyoweza kuwa navyo vituo vya afya vipo vya kutosha kuliko mtu mwingine wambali anapopata.majanga ya afya
About The Author
Last modified: April 9, 2025