Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema Serikali inaendelea kufungua milango kwa wawekezaji wa Biashara ili kuhifadhi mazingira.
Amesema hayo leo Juni 06, 2023 wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora Dkt. Rashid Chuachua pamoja na ujumbe wake waliomtembelea kwa Kuwasilisha taarifa ya kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwa ajili ya biashara ya kaboni.
Ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuhifadhi misitu na nia yao ya kuwekeza katika biashara ya Kaboni akisema kuwa mbali ya kuhifadhi mazingira lakini pia itawa chanzo cha mapato ya halmashauri.
โKutokana na Mikataba ya Kimataifa ya Mabadilkiko ya Tabianchi, sisi kama nchi tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanafaidika na biashara hii na ndio maana tumeandaa kanuni na mwongozo,โ amesema.
Pia, amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ipo tayari kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kuwapa uelewa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini zikiwemo halmashauri kuhusu faida za kupanda miti na kuhifadhi misitu.
About The Author
Last modified: June 6, 2023