Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya walimu mahiri wanaofundisha darasa la awali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) kabla hajafunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Klerruu Iringa.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde
amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kumaliza kero zote
zinazowakabili walimu nchini ili wabaki na jukumu moja tu la kufundisha
kwa umahiri.
Dkt. Msonde hayo mjini Iringa wakati akifunga mafunzo ya walimu mahiri
wanaofundisha darasa la awali yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo cha
Ualimu Klerruu, kwa lengo la kuwapatia ujuzi na maarifa ya kuutekeleza
vyema mtaala wa Darasa la Awali.
Dkt. Msonde amesema, Serikali kwa makusudi imeamua kushughulikia
kero zote za waalimu ndio maana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza waajiri na watendaji wote walio
chini yake kuhakikisha wanamaliza kero zote za walimu nchini.
“Mhe. Mchengerwa amesema hataki kusikia mwalimu yeyote nchini
analalamika wakati Serikali imedhamiria kutatua changamoto zote
zinazowakabili,” Dkt. Msonde amesisitiza.
Kutokana na azma hiyo ya Serikali, Dkt. Msonde amesema walimu wote
nchini wanatakiwa kuwa na jukumu la kufundisha tu ili umahiri utokee na
tija ipatikane katika eneo la taaluma.
“Tunataka walimu wawe na kazi moja tu ya kuhakikisha mnatekeleza
mitaala mipya vizuri ili watoto wapate ujuzi utakaowawezesha kupata
ufaulu mzuri na kutoa mchango katika maendeleo ya taifa hapo baadae,”
Dkt. Msonde amehimiza.
Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kutatua kero za
walimu, Dkt. Msonde ameainisha kuwa zoezi la kutatua changamoto
utofauti wa upandishaji wa madaraja limeshanyika kwa uratibu wa Tume ya
Utumishi wa Walimu na kuongeza kuwa, changamoto ya madai ya
malimbikizo ya mishahara nayo imeshughulikiwa na inaendelea kufanyiwa
kazi na Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Kwa upande wake, mmoja wa washiriki wa mafunzo ya walimu mahiri
wanaofundisha darasa la awali Bi. Sophia Kilavi ameishukuru Serikali kwa
kuwapatia mafunzo ya maudhui ya mtaala mpya wa mwaka 2023
ulioboreshwa ambao wanakwenda kuutekeleza.
Bi. Kilavi amesema wamejifunza kwamba katika ufundisha wa watoto wa
elimu ya awali wanapaswa kutumia vifaa vya TEHAMA vikiwepo
vishikwambi, komputa na Televisheni ili kuwawezesha watoto kumudu
stadi mbalimbali zilizokusudiwa katika mtaala.
Aidha, Bi. Kilavi amesema pia wamejifunza namna ya uchopekaji wa
masuala ya mtambuka ikiwemo elimu ya fedha ya fedha ya kitanzania, utu,
maadili, imani na utamaduni.
Mafunzo haya kwa awamu ya kwanza yamewahusisha jumla ya walimu
1,832 ambao wamegawanyika katika vituo vitano ambavyo ni Chuo cha
Ualimu Kleruu na katika Shule za msingi Gangilonga, Kiesa, Kigambani, na
Njia Panda.
About The Author
Last modified: November 20, 2023