Visit Sponsor

Written by 1:23 pm KITAIFA Views: 41

SERIKALI INAJENGA SHULE MPYA KUTATUA CHANGAMOTO YA WATOTO KUTEMBEA UMBALI MREFU

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akikagua moja ya madarasa yanayojengwa katika Shule ya Sekondari Mputa kupitia mradi wa SEQUIP.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde
amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan inajenga shule mpya nchini, ili kutatua changamoto ya
watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu pamoja na kuondoa
msongamano wa wanafunzi darasani.
Dkt. Msonde amesema hayo akiwa wilayani Namtumbo, wakati akikagua
maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mputa inayojengwa
kupitia fedha za mradi wa SEQUIP.
Dkt. Msonde amesema Serikali haijengi shule kwasababu ya kujifurahisha
au kumridhisha mtu bali inajenga shule kwa lengo la kuwawezesha watoto
wasitembee umbali mrefu kufuata elimu.
“Lengo la Mhe. Rais kujenga shule ni kuwawezesha watoto wa kitanzania
wanaoingia sekondari kumaliza masomo bila kisingizio cha umbali ili
waondoke na ujuzi na umahiri wa kujiletea maendeleo yao pamoja na
kuleta maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla,” Dkt. Msonde
amesisitiza.
Dkt. Msonde amehimiza kuwa, pindi Mhe. Rais akiongeza fedha za ujenzi
wa shule za sekondari, watendaji na viongozi wa kisiasa wajenge shule
kwa kuzingatia kigezo cha utatuzi wa changamoto ya umbali na
msongamano wa wanafunzi darasani na kwenye mabweni.
Aidha, Dkt. Msonde ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Namtumbo kwa kuchagua eneo zuri la kujenga Shule ya Sekondari ya
Mputa na kuongeza kuwa, ujenzi wake ukikamilika vizuri inaweza
kuongezwa adhi ya kuwa na kidato cha tano na cha sita.
Akitoa taarifa ya ujenzi kwa Dkt. Msonde, Mkuu wa Shule hiyo ya
Sekondari Mputa Bw. Godlove Chumi amesema ujenzi umefikia asilimia 71
na mafundi wanaendelea kujenga giblo, kupiga plasta, blundering, kufunga
gypsum board, kupiga koplo, kupachika fremu za mirango na skimming.

Kwa niaba ya bodi ya shule, Kamati ya Ujenzi, Viongozi na Jumuiya nzima
ya Kata ya Mputa, Bw. Chumi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita
kuleta fedha ambazo zinajenga miundombinu ya shule ya Sekondari
Mputa.
Kiasi cha shilingi 560,552,827/= kimetolewa na Serikali kupitia mradi wa
SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari MPUTA, mpaka
sasa kiasi kilichotumika katika ujenzi ni shilingi 379,932,683/= na kiasi
kilichosalia kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ni shilingi 180,620,144/=.

About The Author

(Visited 41 times, 1 visits today)

Last modified: November 21, 2023

Close