Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe, David Kihenzile amekitaka chuo cha taifa cha usafirishaji NIT hakikisha kuwa wanaongeza nguvu na kuwekeza kwenye tafiti hususani eneo la uchukuzi ambalo ndilo lengo la kuanzishwa kwa chuo hicho.
Naibu waziri ameyasema hayo leo Disemba 20 jijini Dar es salaam katika mahafali ya 40 ya chuo cha taifa ch usafirishaji ambapo amewataka wahitimu kuongeza bidii kazi zoa kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
“Wahitimu hawa ni matunda ya kazi yenu nzuri, kwa hiyo dumisheni na kulinda jitihada hizi katika kufikia malengo ya kuwapat wahitimu bora kwa mahitaji ya nchi yetu.” amesema kihenzile
Pia ameuagiza Uongozi wa chuo cha NIT kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika kwa kuwa mahitaji ni makubwa na kuendelea kutumia mapato na ndani katika kuendeleza na kuboresha miundombinu ya chuo.
Ameongeza kuwa serikali ya Rais samia imenunua ndege mbilu kwa ajili ya mafunzo ya urubani na imetoa ardhi katika uwanja wa ndege wa kilimanjaro kwa ajili ya mafunzo ya taaluma za usafiri wa Anga.
Aidha ametoa rai kwa wadau na wafaidika wa shughuli za chuo na taasisi za umma na binafsi kuunga mkono jitihada za chuo hizo katika kupata nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili ziweze kutumi kwa maendeleo ya nchi.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo NIT ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya usajili wa wataalam wa uchukuzi lengo likiwa ni kuwa tambua , kuwasajilu na kusimamka weledi wa maadili ya wataalam wa uchukuzi Tanzania Bara ili kuhakikisha kwamba kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki” amesema naib Waziri.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NIT, Dkt Prosper Magaya amesema wahitimu 4176 wakitunukiwa tuzo mbalimbali kati ya hao wahitimu wakike 1595 ambao sawa na asilimia 38.
“Katika kuhakikisha idadi ya wanafunzi wa kike inaongezeka kwenye taaluma ya uchukuzi n usafirishaji mikakati ya makusudi imewekwa kwenye mapango mkakati wa miaka mitano wa chuo wa mwaka 2021/2022- 2025/ 2026.”amesema Magaya
Pia amewapongeza wahitimu wote wanaotunukiwa tuzo kuanzia Astashahada hadi shahada ya uzamili kuwa wanatambua mafanikio yao juhudi, uvumilivu na kujituma kwao.
About The Author
Last modified: December 20, 2024