Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa
wito kwa Watanzania kujitokeza kutoa maoni kwa ajili ya maandalizi ya Dira ya
Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.
Rais Samia ametoa wito huo leo wakati wa hafla ya kilele cha tamasha la Kizimkazi
lililofanyika katika viwanja vya Kashangae, Paje.
Aidha, Rais Samia amesema Wizara ya Mipango na Uwekezaji kwa kushirikiana na
Wizara ya Fedha zimeanza maandalizi ya dira hiyo ili kupata dira jumuishi yenye
kukidhi mahitaji ya taifa katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Tamasha la Kizimkazi ni la muhimu
kwa wananchi kwa kuwa husaidia kuzinduliwa kwa miradi inayofadhiliwa na wadau
mbalimbali wa maendeleo.
Rais Samia pia ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na
serikali kupunguza na kuondoa changamoto zinazoendelea kujitokeza katika mkoa
wa Kusini.
Vile vile, Rais Samia amesema serikali ina mpango wa kutekeleza mradi wa Jenga
Kesho iliyo Bora visiwani Zanzibar ili kuwawezesha vijana wengi kujiajiri mkoani
humo.
Hali kadhalika, Rais Samia amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili
kufanikisha harakati za kuleta maendeleo ya uchumi kwa maslahi ya jamii na taifa
kwa ujumla.
About The Author
Last modified: September 1, 2023