Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
TAMASHA la Samia Fashion Festival linatarajiwa kufanyika Oktoba 27,2024 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Oktoba 11,2024 Jijini Dar es Salaam,Muanzilishi na Muandaaji wa Tamasha la Samia Fashion Festival Khadija Mwanamboka amesema kwamba tamasha hilo litahusisha watoto kuanzia umri wa miaka 7 Hadi 17 ili waweze kuonyesha vipaji vyao.
Mwanamboka ameeleza kwamba tamasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na maono yake na ni heshima kwa uongozi wake katika kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi hasa katika sekta ya ubunifu.
“Tamasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na limelenga kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi Hulu likionyesha mchango wa Rais katika sekta ya ubunifu.Tamasha litaendelea kwa siku Saba,likijumuisha matukio mbalimbali ya kuwawezesha wanawake,watoto na vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar”,amesema
Aidha kauli mbiu ya tamasha hili ni”Ubunifu na Stara” ikiwa ni taswira tosha ya nafasi na haiba ya mama yeti mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na kwa jinsi Gani jamii inaweza kutumia haiba hiyo yenye stara katika nyanja mbalimbalo za kijamii kama vile motiko,sherehe ,shughuli za jioni ,malezi na kadhalika.
“Tamasha hili si sherehe ya mavazi tu, ni jukwaa la kuonyesha ubunifu wa Kitanzania na ni heshima kwa uongozi na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan “,amesema Khadija Mwanamboka .
Aliongeza kwamba anawakaribisha wabunifu wote kwa mikoa yote ya Tanzania kushiriki fursa hii kwa kutuma kazi zao na jopo la majajo mahiri na wazoefu katika sekta ya mitindo wakiongozwa na Chief Judge mwanamitindo Miriam Odemba ,Mwanamitindo wa Kitanzania anayeishi Ufaransa.
About The Author
Last modified: October 12, 2024