Visit Sponsor

Written by 2:08 pm KITAIFA, Uncategorized Views: 19

SAID FELLA: TUNAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUTUJENGEA DARAJA KILUNGULE

Na Carren Mgonja

WANANCHI wa kitongoji cha Kilungule na maeneo ya jirani, Dar es Salaam wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea daraja linalowawezesha kupita kwa urahisi kwenda na kurudi kwenye shughuli zao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Jumatatu Juni 3, 2024, Diwani wa Kata hiyo, Saidi Hassan Fella ‘Mkubwa Fella’ alisema kuwa awali baadhi ya shughuli zao zlikwama kutokana na ubovu wa daraja Hilo.

“Mvua ikinyesha miezi kibao hatupiti na hivyo kuathiri kipato chetu, kwa upendo aliotuonyesha mama, kwa kweli tunashukuru Mungu na tunamuombea adumu sana”, alisema Fella.

Aidha Alisema kuwa wananchi wake na majirani wa kitongoji hicho wamemtuma diwani wao kwenda kwa mama na kumshukuru?. Alisema Fella.

(Visited 19 times, 1 visits today)

Last modified: June 5, 2024

Close