Visit Sponsor

Written by 4:33 am KITAIFA Views: 8

REA YAUPAMBA MKUTANO WA KIKANDA WA NISHATI BORA 2024

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

Matumizi bora ya nishati ya kupikia kupewa kipaumbele

Elimu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme yatolewa

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unashiriki katika Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati 2024 unaofanyika jijini Arusha  ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

REA imeungana na wadau  mbalimbali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo (SADC) kushiriki katika mkutano huo muhimu.

Aidha, wadau mbalimbali wameendelea kuvutiwa na huduma zinazotolewa katika banda la REA ikiwemo elimu sahihi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.

Kupitia mkutano huo, REA imetoa elimu kwa wadau mbalimbali wa nishati ya umeme ili kuwahakikishia Watanzania upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.

About The Author

(Visited 8 times, 1 visits today)

Last modified: December 5, 2024

Close