Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko amempongeza, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinis alivyoimarisha uchumi, kwani kwa kipindi cha miaka minne ametoa zaidi ya Shilingi Trillion 1.56 kwa ajili ya shughuli za maendeleo mkoani hapo ambazo pia zimesaidia kuimarisha sekta ya nishati, zaidi ya 80% maeneo ya mjini yanapata umeme na 70% vijijini, huduma za afya na miudombinu ya usafirishaji imeimarishwa.
RC Mlindoko aliyasema hayo jana Aprili 3, 2025 wakati akizindua zoezi la mafunzo na uibuaji wa miradi yenye mvuto wa ubia (PPPs) linaloendeshwa na kituo cha Ubia (PPPC) Tanzania inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri zake ambapo wataalam 42 wamepatiwa mafunzo hayo.
Mhe. Mrindoko amempongeza Dkt. Samia kwa kuanzisha kituo cha ubia (PPPC) na kuitaja hatua hiyo kama hatua ya kijasiri kwani kazi inayofanywa na kituo cha ubia chini ya Ndg David Kafulila ni ya mfano, sasa dhana ya ubia inaanza kueleweka nchini.
Mafunzo hayo yanayoratibiwa na wakufunzi Dr. Bravious Kahyoza na Michael Kihanga yana malengo muhimu yafuatayo;
1)Kuelewa dhana ya PPP na kuibua miradi yenye sifa ya utekelezwaji wa ubia.
ii).Kuandaa maandiko dhana (Project Concept Notes)
iii)Kuandaa matangazo ya miradi kwa wawekezaji
Kutumia teknolojia ya GIS katika uwekaji wa miradi kwenye ramani za Halmashauri
Kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhe. Mrindoko alieleze kuwa mkoa wa Katavi ni mkoa wenye fursa lukuki za kiuwekezaji ambazo zina mvuto wa ubia na kuzitaja fursa hizo ni kwenye sekta ya mazao ya misitu kama ufugaji wa nyuki, utalii unaohanikizwa na mbuga ya Katavi, uvuvi, usafirishaji na sekta ya kilimo.
“Hatua hizi za uwekezaji kwenye miundombinu zitakuwa muhimu kwenye miradi ya PPP mkoani Katavi”, alisema.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Ndg. Albert Msovela amesema mafunzo hayo yatakuwa na msaada mkubwa wa mkoa wa Katavi na kusisitiza kuwa mkoa uko tayari kushirikiana na PPPC kwenye shughuli za ubia.
PPPC inaendelea kutoa mafunzo katika mikoa 13 nchini kwa ajili ya uibuaji wa miradi ya PPP kwa maendeleo ikiwa ni awamu ya pili ya zoezi hili.
PPPCentre #PPP #Ubia #Katavi #Uwekezaji #Mafunzo #Maendeleo


About The Author
Last modified: April 3, 2025