Visit Sponsor

Written by 9:30 am KITAIFA Views: 28

RC KAGERA ATAKA NGUVU YA PAMOJA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa akiwahutubia Wananchi wa kata ya Ruzinga Wilayani Misenyi katika maadhimisho ya maendeleo ya kata hiyo maarufu Ruzinga Day

Na Lydia Lugakila, Misenyi

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewaomba Wananchi katika kata ya Ruzinga Wilayani Misenyi na Wana Kagera kwa pamoja kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka
hii ikiwa ni baada ya kutoridhishwa na ufaulu kwa miaka mitatu iliyopita.

Hajat Fatma Mwassa ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia Wananchi wa kata ya Ruzinga katika maadhimisho ya siku ya maendeleo ya kata maarufu Ruzinga Day.

RC Mwassa amesema kuwa licha ya umoja wa wadau wa maendeleo ujulikanao kama Ruzinga Development Association(RD) kujipambanua katika nyanja mbali mbali zikiwemo za maendeleo katika kata ya Ruzinga ikiwemo ujenzi wa shule Sekondari ya Ruzinga,ujenzi wa nyumba za Walimu shule ya Msingi Ruzinga, ujenzi wa Bweni la shule ya Sekondari Ruzinga, ujenzi wa vyumba vya madarasa na Ofisi za Walimu shule ya Msingi Ruhija pamoja na miradi mingine huku akitaka suala la ufaulu lionyeshe mabadiliko ya haraka baada ya kuonyesha mkwamo kwa muda mrefu.

“Tumeona wana RD mlivyoonyesha maendeleo makubwa sana ya kimaendeleo kupitia michango mbali mbali lakini nitangaze kwa masikitiko kwa miaka mitatu iliyopita kiwango cha ufaulu kwa Mkoa wa Kagera katika historia kwa mara ya kwanza kimeonekana Kushuka hili ni jambo la kupingwa kwa nguvu zetu zote” alisema RC Mwassa.

Amewaomba Wana Ruzinga na Wanagera kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja kulikataa suala hilo la Kushuka kwa Elimu.

Aidha amesema kuwa Kushuka kwa Elimu kwa kiasi kikubwa kunaashiria wazi uzembe wa watendaji katika sekta ya Elimu huku akiahidi kuwa kwa mwaka huu wa 2024 atahakikisha anaweka msukumo mkubwa ili kiwango cha elimu kipande kwa kwa haraka ndani ya miaka miwili ijayo.

Hata hivyo alisisitiza kuwa kila mmoja kwa wakati wake atimize wajibu wake ambapo ameahidi mageuzi makubwa ili elimu irudi katika upya katika nafasi ya ufaulu wa uliokuwepo awali.

About The Author

(Visited 28 times, 1 visits today)

Last modified: January 3, 2024

Close