Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albart Chalamila amewataka Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo Mtaa wa Kongo na Msimbazi kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo juhudi za uokoaji zikiendelea kwenye ghorofa lililoanguka leo asubuhi.
Aidha, amesema kuwa jengo hilo lina maduka na stoo za kuhifadhia bidhaa, ambapo mpaka sasa wamekwisha okoa badhi ya majeruhi wa tukio hilo na kuwapaleka katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, huku Kikosi cha Zimamoto, Jeshi la Polisi, Watoa huduma ya kwanza kutoka Hospitali ya Muhimbili na Wananchi waliendelea na juhudi za kuokoa watu wengine walionasa katika katika ghorofa hilo.
” Kuhusu taarifa ya kiwango gani cha majeruhi ama kuna vifo kutokana na ajali hii tutaendelea kuhabarishana, lakini mpaka wakati huu hali ya kiusalama ni kubwa sana, niwaombe wafanyabiashara wote, ndugu na jamaa, marafiki zao na wote ambao wapo katika eneo hili tuendelee kuwa na subira kwani tumefanya jitihada za kuleta mitambo ya uokoaji, “
” Nyie mnafahamu Greda au Skaveta haliwezi kupita barabarani mpaka libebwe na lowberd ambalo ni gari maalumu la kubeba mitambo, na kwa muda huu lipo karibu na hapa kuja kufanya maokozi, niwatoe watu wote wasiwasi kuwa Polisi kazi yao ni kulinda amani katika maeneo haya, ku rescue ni kazi inayofanywa na kikosi maalumu, ” amesema Chalamila.
Ameendele kusema kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa watu wote ambao wamepatwa na janga hili kwa kuharibikiwa au kupotea kwa mizigo yao, kujeruhiwa kwa ndugu zao, jamaa au rafiki zao na hata mwenye jengo.
“Nitoe Rai kuwa wakati huu si muda wa kulaumiana nani amesababisha, sasa ni muda wa kuokoa wenzetu, maana jengo hili lina underground ambapo tunaambiwa kuwa wapo pia watu huko, baada ya muda tutatoa taarifa sahii ya wangapi wamejeruhiwa na wangapi wanahali gani, wangapi wamefikishwa hospitali, nihitimishe kwa kusema kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, uokoaji, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Kamati za Usalama na Uokoaji, tunaye Prof Janabi kutoka Hospitali ya Muhimbili ambaye ni mkurugezi pale na tunazo ambulance hapa za kubeba majeruhi,” akisema Chalamila.
Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi Dar es Salaam Jumanne Murilo amewaomba wananchi wote walio panda katika majengo ya jirani kushuka na kuacha kupiga picha za eneo hilo kwani kuwa karibu na jengo hilo ni hatari kwao maana bado linaning’ia hivyo linaweza kupolomoka na kuwaletea madhara
About The Author
Last modified: November 16, 2024