Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI
Kwa kuelekea siku ya wanawake duniani kwa tamko la Beijing linalotimiza miaka 30 Kwa kusheherekea siku ya wanawake duniani Ambapo kilele chake kufanyika siku ya Tarehe 8 Machi
Mapinduzi ya Beijing yaliyoanza kufanywa mwaka 1995 Hadi siku ya Leo yanamueka mwanamke kama mtu mwenye mchango sawa na Mwanaume Katika uongozi,Siasa, Uchumi na Katika maswala yote ya kiutamaduni ikiwa pamoja na kuzifuta baadhi ya tamaduni ambazo zimekuwa na mchango mkubwa sana wa kumzuia mwanamke kutokwenda mbele

Tunapomzungumzia mwanadamu mwenye tija Katika Taifa mwanamke alikuwa Wala haesabiki kama ni mtu anaeweza kuwa na tija Katika Taifa
Mkoa wa dar es salaam umeweza kupanga kazi kadhaa ambazo zitafanyika kabla ya siku ya Tarehe 8 Kwa kuwatambua wanawake na kuwapa kipaumbele kikubwa Katika siku hiyo ya wanawake duniani

Ameyasema hayo Leo Tarehe 3 Machi 2025 mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila Amesema Tarehe 4 machi kutakuwa na kongamano kubwa la wanawake ambalo litakuwa limebeba dhima au kauli mbiu isemayo ni “ushiriki na mchango wa makundi maalum Katika kufikia fulsa za uwewezeshaji kiuchumi kuelekea miaka 30 ya Beijing”
Kongamano hilo litafanyika Katika ukumbi wa ubungo plaza aidha chalamila ameweza kutoa Rai Kwa wanawake wote kuweza kuhudhuria Katika kongamano hilo na mgeni rasmi atakuwa professor kitila mkumbo

Aidha chalamila Amesema sherehe hizo za wanawake duniani kitaifa zitafanyikia jijini Arusha na mkoa wa dar es salaam zitafanyikia Katika viwanja vya leader club siku ya Tarehe 8
“Moja Katika shughuli zitakazo fanyika Katika siku hizo za wanawake kutakuwa na kugawa mitungi ya gesi Kwa akina mama ambao Kwa Muda mrefu wamelia sana Kwa kutumia nishati chafu ambayo imeleta madhara makubwa ya afya zao na Total energy wametoa mitungi Elfu Moja watayoigawa kuazia kesho Tarehe 4 mpaka kilele Cha maadhimisho hayo”. Amesema chalamila

Chalamila Amesema tamko la Beijing Kwa sehemu kubwa liligusa Zaidi kumwinua mwanamke na kumfanya kuwa kiumbe chenye mchango mkubwa Katika ulimwengu wote Katika maendeleo hapa duniani na tunahaki ya kujivunia Katika utawala wa Dkt Samia Suluhu Hassan ambao ni kielelezo Cha kwanza kikubwa kwamba mwanamke ameshafikia hatua kubwa Katika Taifa letu Kwa kuwa kiongozi namba 1
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kutambua umuhimu wa Beijing Declaration tangu mwaka 1995 aliamua kuunda wizara maarum ambayo inayoitwa WIZARA ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maarum ambayo wizara hiyo ipo chini ya waziri Dorothy Gwajima na ambae ndio amekuwa mwaandaaji namba 1 Katika kongamano hilo

“Tunaposheherekea sherehe hizi za wanawake wote duniani tunatambua ya kwamba Katika mnyororo huo wa thamani ya kusheherekea mafanikio makubwa ya wanawake duniani nasi wanaume tunapaswa kuwa na mchango mkubwa wa kuhakikisha dunia na Tanzania Kwa ujumla tunafikia Katika jendA ikwaliti”Ameongeza chalamila
Halikadhalika chalamila Amesema Tunapoelekea sikukuu hizi za wanawake duniani kote ni dhahiri kwamba Moja ya agenda yetu tuliyokuwa nayo ni kuhakikisha tunaendelea kuwezesha mwanamke kiuchumi Ili aweze Kuendelea kuwa Katika sehemu ya tija kubwa Katika Taifa letu
Kauli mbiu siku ya Tarehe 8 ni maadhimisho ya siku ya mwanamke Kwa mwaka 2025 mwanamke na wasichana 2025 tuimalishe haki usawa na uwewezeshaji
About The Author
Last modified: March 3, 2025