Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira (DAWASA) Mkoani humo kuanza mchakato wa kuzalisha umeme utakaotumika katika mashine za kusambazia maji ili kupunguza gharama.
RC Chalamila ametoa magizo hayo mapema leo April 9,2025 wakati akikagua mradi wa kituo cha kusukuma maji Kibamba Luguruni ambao umegharimu Shilingi billioni 36.8,ambapo kwa Kibamba ukiwa umetumia bilioni 4.
Aidha amesema kwamba kwa sasa DAWASA inatumia bil. 2 kulilipa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa ajili ya bili ya umeme,hivyo gharama hiyo inaweza kuepuka ikiwa itazalisha umeme wake na Tanesco itumike kusambaza pekee.

“Sisi tunapoona mradi huu umeanza kufanya kazi ,ni mafanikio makubwa na tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ambao utatoa huduma ya maji kwa Watanzania wengi” amesema
Nakuongeza kuwa “Hivyo huu si muda wa kudanganyana kama kuna tatizo sehemu kiongozi husika anatakiwa kusema ili Serikali itoe fedha, nikigundua kuna kiongozi hajasema ukweli kama kuna tatizo sehemu ili wananchi wasaidiwe na nikabainika nitaanza na yeye,”.amesisitiza Kiongozi huyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,, Lazaro Twange, amesema kwamba kukamilika kwa mradi wa maji Kibamba kumefanikisha kuondoa changamoto ya ukosefu ya maji katika Kata za jimbo hilo.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Kwembe, Bw.Nicolus Batiligaya amesema mwaka 2020, kata yake ilikuwa na ukosefu wa maji na sasa wananchi wake wanapata huduma hiyo kwa asilimia 90.
“Namshukuru sana Rais Dkt.Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ujenzi wa miundombinu ya maji ambayo imeboresha maisha ya wananchi wangu kupata maji safi na salama na kuwepo utofauti mkubwa na miaka mitano iliyopita, ” amesema Batiligaya.
About The Author
Last modified: April 9, 2025