Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI g
-Asema Serikali imeshapima viwanja zaidi ya 2274.
-Awataka wale wote waliovamia na kujenga kulipia viwanja hivyo mara moja kwa kuwa wamepunguziwa bei.
Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kutaka waliovamia na kujenga kwenye eneo linalomilikiwa na shirika la maendeleo Dar es Salaam (DDC) lililopo Mabwepande kuuziwa viwanja kwa gharama nafuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila kwa kushirikiana na shirika hilo pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni ametangaza rasmi rasmi kuanzaย kuuza viwanja katika eneo hilo
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8, 2025 eneo la Mabwepande akiwa ameambatana Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, viongozi wa DDC pamoja na wataalamu wa ardhi kutoka Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni RC Chalamila amesema eneo hilo lenye viwanja zaidi ya 2274 vyenye ukubwa tofauti tofauti ambavyo baadhi vilivamiwa na vingine havijavamiwa viaanza kuuzwa rasmi.
Aidha RC Chalamila amesema kuwa viwanja hivyo vianze kuuzwa mara moja kuanzia wiki ijayo ambapo wananchi waliovamia kwa miaka mingi na wapo kwenye eneo hilo watauziwa kwa gharama ya shilingi elfu tatu kwa mita ya mraba wakati wengine watakaohitaji viwanja watauziwa kwa shilingi elfu 15,17 na 20 kwa mita ya mraba kulingana na matumizi yake kama makazi biashara au matumizi mengine
Vilevile RC Chalamila amewaeleza wananchi wa eneo hilo na ambao watanunua viwanja kuwa Rais Dkt Samia ameshapeleka huduma muhimu za kijamii kwenye eneo hilo ikiwemo umeme na maji na kwamba barabara ipo kwenye mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami kupitia TANROAD
Kwa upande wa Afisa mipango miji Manispaa ya Kinondoni Arkadius Haule amewahakikishia wananchi kuwa viwanja hivyo vyote vimepimwa na vitauzwa kwa kuzingatia uhitaji wa mnunuzi huku Ali Mirambo Meneja Mkuu wa DDC akiwahakikishia wananchi kuwa eneo hilo ni mali ya shirika hilo hivyo wanauziwa na mmiliki halisi
About The Author
Last modified: February 9, 2025