Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma Julai 8, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT yatakayofanyika Julai 10, 2023 jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo Julai 8, 2023 jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.
“Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT kinatarajiwa kuadhimishwa rasmi ifikapo tarehe 10 Julai, 2023. Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nipende kutumia fursa hii kuwaalika viongozi wote wa Serikali, Taasisi mbalimbali za umma, na binafsi,

Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo
watumishi, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla, kujitokeze kwa wingi kuhudhuria siku ya kilele cha maadhimisho haya“, alisema Mhe. Bashungwa.
Pia, aliwashukuru wadhamini na wote walioshiriki katika maandalizi ya Miaka 60 ya JKT ikiwa ni pamoja na uongozi wa Mkoa wa Dodoma, chini ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Staki Senyamule kwa uratibu unaoendelea katika kufanikisha maadhimisho hayo ya kihistoria.
Awali, Mhe. Bashungwa alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassankwa jitihada anazozifanya za kuhakikisha JKT inaendelea kuwa kitovu cha malezi bora kwa vijana wa kitanzania.
About The Author
Last modified: July 8, 2023